Cover Image
close this bookUtangulizi wa Lugha na Isimu (Tanzania Publishing House Dar Es Salam, 1994, 121 p.)
close this folderSura ya Kwanza: Ujuzi wa Lugha
View the document1.0. Utangulizi
Open this folder and view contents1.1. Kujua Lugha ni nini?
Open this folder and view contents1.2. Isimu ni Nini?
View the documentMazoezi

Mazoezi

1. Angalia sentensi zifuatazo:

i) Wanafunzi walioingia Chuoni mwaka huu ni hodari sana
ii) Wazazi wamekuja wa Mwajuma na Ali
iii) Kama ukitueleza tulikusikia
iv) Kwa nini hukuleta vitabu tulivyokuagiza vya hadithi?
v) Asiyesikia la mguu utavunjika guu

Jibu maswali yafutayo:

a) Sentensi zipi unazikubali haraka bila matatizo?
b) Zipi unazikubali kwa mashaka? Kwa nini?
c) Zipi unazikataa kabisa? Kwa nini?

2. Katika lugha kuna maneno ambayo yanachukua maana zake kutokana na mlio wa vitu yanavyovitaja:

a) Orodhesha maneno yasiyopungua kumi ya namna hiyo kutoka Kiswahili.
b) Je, kuna utaratibu maalumu unaotumika katika “kuunda” maneno hayo?
c) Katika lugha nyingine unayoijua, maneno hayo yana maumbo gani? Unayalinganishaje na hayo ya Kiswahili?

3. Wanadamu wanatumia njia nyingine za mawasiliano mbali ya lugha:

a) Eleza njia mbili za mawasilianu zisizotumia lugha, na jinsi zinavyotumika.
b) Njia hizo zinaweza kutumika badala ya lugha? Eleza.

4. Angalia sentensi zifuatazo:

i) Maneno ya Juma yamenifurahisha sana
ii) Lugha ya Juma leo imenifurahisha sana
iii) Maneno ya sentensi hii ni magumu sana

Kuna uhusiano gani kati ya “maneno” na “lugha” katika semi hizi?