
| Utenzi wa Nyakiiru Kibi (ECOL Publications, 1997, 109 p.) |
|

Taswira
615
Habari ilienea
Watu wakaisikia
Kawamara
wametua
Vijana wa kuvutia.
616
Wana mioyo ya wema
Wanagawa bure nyama
Na adabu na
heshima
Na nguo wamevalia.
617
Kwa kasi ilisambaa
Habari ikazagaa
Watu wakaja
manria
Wageni kuangalia.
618
Habari ikasaflri
Hadi katika kasiri
Ya Omukama
amiri
Ntumwa akaisikia.
619
Akataka sulutani
Waitwe mara wageni
Kuwahoji
atamani
Ajue walichojia.
620
Akapelekwa tarishi
Mwenye mbio mtumishi
Aupeleke
utashi
Wa mkuu wa jamia.
621
Mithili ya mbayuwayu
Akenda mjumbe huyu
Anahema
kama kuyu
Kwa mbio kuzidmua.
622
Kwake Nyakiru mgeni
Kabisha kangia ndani
Akisha
subalherini
Amri kaitongoa.
623
Mtukufu Omukama
Simba anayenguruma
Mume wa
waume wema
Wageni awamkia.
624
Mtukufu wajamala
Anasema halahala
Leo
msende kulala
Kabula ya kumwendea.
625
Mtukufu utashiwe
Leo mfike mpewe
Atakayo
muambiwe
Na kisha mtarejea.
626
Akaridhi muungwana
Twashukuru maulana
Tu
watumwa wake bwana
Wito twauitikia.
627
Kamwita Kanyamaishwa
Kumwarifu alopashwa
Kuwa
wameamrishwa
Kigarama kwelemea.
628
Wakawaita wenzao
Kuwapa ujumbe huo
Wafanye
maandalio
Ikuluni kwelekea.
629
Wakavalia vizuri
Ngozi zisizo dosari
Wakisha kuwa
tayari
Safari wakabandua.
630
Wakaenda kishujaa
Silaha zang'aang'aa
Kigarama
wakangia
Mukama kawapokea.

Taswira
631
Wapi mlikotokea
Wapi mnakokwendea
Kazi gani
mwafanyia
Kujua natamania.
632
Wakamjibu vijana
Twasikia maulana
Nasi tu
radhi kunena
Yote kukutobolea.
633
Sisi, ewe Mtukufu
Tu wawindaji hafifu
Nasaba
zetu dhaifu
Tu wanyonge twazagaa.
634
Twazagaa e Jalali
Karibuni hata
mbali
Tukitafuta fadhili
Nyakiru akatongoa.
635
Kibumbiro ni nyumbani
Kiziba sisi wageni
Bali
tunayo imani
Simba utatujalia.
636
Kuwinda ni kazi yetu
Toka utotoni
mwetu
Kuivinjari misitu
Ndiyo ya kwetu tabia.
637
Twajua kila mnyama
Kila ndege mwenye nyama
Na
misimu ya kuhama
Ya madege twaijua.
638
Twajua misitu gani
Husitawisha
kongoni
Kuro, swala hata nyani
Makazi yao twajua.
639
Twajua kila kiumbe
Toka kwa simba
kabambe
Hadi kwa fisi mzembe
Mahiri wa kudoea.
640
Tunajua tamu nyama
Hutoka yupi mnyama
Na
nyama ngumu kuuma
Mnyama gani hutoa.
641
Tu mafundi wa kuvuta
Kila aina ya nyuta
Pia
mapanga kufuta
Na mikuki kuinua.
642
Japo tu watu hafifu
Sio watu wenye hofu
Japo
sio watukufu
Uungwana twaujua.
643
Tumezurura kutosha
Kadka yetu maisha
Twapenda
kubahatisha
Maisha yalotulia.
644
Kwa fadhilazo mwadhamu
Tu radhi kuishi
humu
Tufanye masitakimu
Na kuwa zako raia.
645
Tu radhi kutumikishwa
Tu radhi
kuamrishwa
Hili litahakikishwa
Muda ukitupatia.
646
Sisi na wetu vijana
Tuko radhi kupigana
Ili
kudumisha jina
La enzi yako murua.
647
Hatuogopi adui
Katika dunia hii
Madhali bado
tu hai
Huna cha kukihofia.
648
Vita ni chakula chetu
Damu ni kinywaji
chetu
Adui zako ni zetu
Wajapo watatujua.
649
Nchi hii ya Kiziba
Ni nchi yenye haiba
Wana
bahati Baziba
Humu wanaolowea.
650
Una bahad Mukama
Kutawala nchi njema
Yenye
maziwa na nyama
Kama hii twakwambia.
651
Kwa kuwa twaitamani
Tu radhi
kuiauni
Ukikiri masikani
Yetu hapa kujengea.
652
Akiyasikiya haya
Mukama kafurahiya
Kaona siyo
wabaya
Hawa wawinda shujaa.
653
Kakuna upara wake
Na ndevu na mvi zake
Kasugua
bongo zake
Kaona watamfaa.
654
Kaona watamfaa
Wataja mpigania
Nchini
akiridhia
Kuwaruhusu kukaa.
655
Watoto wake wachanga
Wanaonyesha ujinga
Wataogopa
mapanga
Hapo watakapokua.
656
Watakaposhika enzi
Watahitaji
walinzi
Wapepezi na wakanzi
Ili kuwahudumia.
657
Kwani uzee balaa
Kaona unamtwaa
Ujana
wamuambaa
Yazimika yake taa.
658
Na hivyo akatamka
Ombi limekubalika
Mwaweza
kujenga maka
Kizibani kulowea.
659
Nawapenda wanaume
Wenye nyoyo za kiume
Na
maungo ya kidume
Kuja kunitumikia.
660
Napenda waume bora
Wasochelea madhara
Walo
tayari kukera
Adui kuniulia.
661
Mnaweza kwendelea
Makazi kujijengea
Kibali
nimekitoa
Hamna cha kuhofia.

Taswira
662
Wakamshukuru sana
Hilo alipolinena
Na kuhakikisha
tena
Kuwa watamfalia.
663
Kwa furaha wakatoka
Waongea na kucheka
Kwani
wamekubalika
Kadka nchi kukaa.
664
Wakirudi majumbani
Wakaweleza wandani
Mambo yote
Kikaleni
Ambavyo yamewendea.
665
Pia wakawaambia
Wake zetuni sikia
Mnaweza
kupania
Mashamba kujilimia.
666
Kama wanawake wote
Mabibi nchini
popote
Mlime, maji mchote
Hamna cha kuhofia.
667
Udongo mwanze kuchimba
Tupandikize
migomba
Mpalilie mashamba
Na ndizi kujichumia.
668
Utapofika msimu
Wa maharage matamu
Mpande ili
kukimu
Wa'me zenu na jamaa.
669
Sisi waume vijana
Kuwinda hatutakana
Tutazidi
kupambana
Na nyang'au wa dunia.
670
Tutazidisha usasi
Wa nyama bila
kiasi
Tujiletee nemsi
Na kuwalisha raia.
671
Pia tutajizoeza
Mishale kuipaaza
Na panga
kuzipepeza
Na mikuki kurushia.
672
Tufanye jeshi la nguvu
La wachache wa
mabavu
Kuja kufuta maovu
Ambayo yamezagaa.
673
Na kwa kwandalia hili
Mwendo hawakubadili
Raha
hawakukubali
Tabu walivumilia.
674
Waendelea kuuwa
Wanyama wanaoliwa
Na nyama yao
kugawa
Kwa wakulima raia.
675
Wauwapo kwa upanga
Nyama mmoja mjinga
Hukata na
kumchonga
Watu wakawagawia.
676
Hivyo wakajulikana
Kwa wazee na vijana
Watumwa na
waungwana
Wote wakawasifia.
677
Wakasema Hawa watu
Ni kama wazazi wetu
Bahad
kwa nchi yetu
Kuwa wameijilia.
678
Hawa kwetu walishaji
Matumbo
washibishaji
Wagawi si wafujaji
Mengi wastahilia.
679
Nyama ikawa nchini
Kama ndizi za shambani
Watu
wakawa rahani
Kwa nyama kuwazidia.
680
Mifugo haWakuchinja
Nyama yao kuionja
Ng'ombe
mazizi wavunja
Jinsi walivyozidia.
681
Watu wakatajinka
Maziwa yakafurika
Nyama
zikamiminika
Nchini zikaenea.
682
Ukanong'ozana umma
Wameileta neema
Hawa
wawindaji wema
Mizimu wawape dia.
683
Nyamuhanga wabariki
Waondokane na
dhiki
Wape mali kwa malaki
Waitawale dunia.
684
Wape faraja Mugasha
Uwaepushe
rabusha
Nyakalembe wa maisha
Uwaepushe na njaa.
685
Irungu wape salama
Washinde kila
mnyama
Tuzidi kula minyama
Miungu twawalilia.
686
Na huu wote wakad
Mutalala ameketi
Nyumbani kama
hayati
Akila ha kujinywea.
687
Kachutama kama nguu
Ashindwa kwinuka juu
Au kwinua
mguu
Unene wamzidia.
688
Unene wamzidia
Kama kameza dunia
Na bado
ajipakia
Vyakula kwa magunia.
689
Ulezi vyungu na vyungu
Na matoke kwa mikungu
Vitamu
hata vichungu
Kinywanimwe hupotea.
690
Maziwa yenye shahamu
Maji yenye chumvi
tamu
Mapombe nayo dawamu
Huyanywa akibugia.
691
Dunia ina mizungu
Imewazua wazungu
Na
Mutalala mwenzangu
Yu mzungu nakwambia.
692
Mzungu hawezi shiba
Japo angemeza mamba!
Nguruwe
katika shamba
Zimwi kadka dunia.
693
Akisha kula bahau
Ngoma aliisahau
Ameshapata
nafuu
Ya tumbo kujijazia.
694
Nafuu amesha pata
Kitambi kimeshaota
Kwani kuanza
matata
Goma shinda kuwania?
695
Hajui kushika panga
Wala ngao kujikinga
Vita kwake
ni ujinga
Kwani kuvifuatia?
696
Ndivyo alivyoamini
Mutalala ugenini
Na hii yake
imani
Vema alishikilia.
697
Wenzake aliwacheka
Kuona wanatumika
Misuli
yajisimika
Matumbo yawabonyea.
698
Maisha ni kula sana
Na kunywa kulewa sana
Na
kujizalia wana
Na mwishowe kujifia.
699
Kamwe si kutangatanga
Kama nzige kwenye
anga
Bila makazi kujenga
Na tumbo kujilelea.
700
Ndivyo alivyowambia
Mutalala asojaa
Na sasa
twamuachia
Yake tumeyasikia.
701
Yake tumeyasikia
Sasa tuzidi kujua
Nyama za wale
shujaa
Nini zilichokizaa.
702
Kwanza na itambulike
Ile Ngoma ya
makeke
Kachwankizi Ngoma pweke
Nyakiru aliitwaa.
703
Nyumbani kaisetiri
Aitunza kwa hadhari
Kuigusa ni
hatari
Japo uwe Malikia.
704
Kachwankizi imetua
Hapo imejiketia
Kwa
saburi yangojea
Siku yake ya kung'aa.
705
Sasa basi siku moja
Asubuhi ilikuja
Habari yenye
faraja
Watu kuwaamkia.
706
Ikaingia habari
Mapema alifajiri
Habari kweli ya
heri
Senene wameingia.
707
Senene wameingia
Mithili wingu la mvua
Kwa
wingi wamezidia
Enyi Baziba sikia.
708
Enyi Baziba wafane
Enyi walaji
senene
Tokeni nje muone
Alichotuangushia.
709
Alichotuangushia
Mugasha mwenye
kujua
Asiyeogopa jua
Mweusi mleta mvua.
710
Tokeni nje mabibi
Wanaume hawashibi
Leo hadi
magharibi
Wajazie magunia.
711
Tokeni nje madume
Uzembe wenu ukome
Senene
muwaandame
Jioni watajendea.
712
Tokeni nje watwana
Na mihi yenu
vijana
Lete senene kwa bwana
Sulutani kujilia.
713
Tokeni nje watoto
Acheni zenu
topito
Kuna mlo motomoto
Washika na kujilia!
714
Na watu wakaondoka
Kila hirimu na
rika
Senene kwenda kusaka
Katika zogo la mvua.
715
Watu wakajifunika
Milumba yenye viraka
Na ngozi
wakajivika
Manyuriyu kuyazuia.
716
Na maji yakaanguka
Kwa ghadhabu ya kizuka
Aridhi
ikafurika
Mifuo yakachimbua.
717
Meme zinamemetuka
Radi nazo zapasuka
Nchi
inatetemeka
Kama ukufi sikia!
718
Wasijali binadamu
Wenye shauku na hamu
Kupata
senene tamu
Tumboni kujitilia.
719
Wakajitoma sharini
Kwa ari iso kifani
Na
kuyalaza majani
Senene kujishikia.
720
Senene bila vitimbi
Wakaangnka kiwimbi
Wimbi
baada ya wimbi
Watu wakajizolea.
721
Senene kawa senene
Kila mahali senene
Kushoto kwako
senene
Mbele nyuma na kulia!
722
Kichwani pako senene
Nyayoni pako senene
Nguoni
mwako senene
Senene wakazagaa!
723
Katika nyasi senene
Kadka miche senene
Na mitini ni
senene
Senene wakaenea.
724
Senene kwenye mashamba
Senene kwenye miamba
Kwenye
mapaa ya nyumba
Senene wakatambaa!
725
Senene miti kishika
Matawi yanavunjika
Matunda
yanaanguka
Na mashina kupembea!

Taswira
726
Nyumba wakiikalia
Hubonyeza lake paa
Na ndani
wakiingia
Nyumba wanairarua!
727
Ndivyo walivyoanguka
Hao senene wa
mwaka
Wakazidisha mpaka
Jinsi walivyoenea.
728
Kabula ya siku hio
Senene kwa wingi
huo
Hawajakumbana nao
Kiziba kuangukia.
729
Pia tangu siku hio
Watu wanakiri leo
Senene wengi
ja hao
Katu hawajatokea.
730
Ntumwa katika nyumbaye
Kuona senene naye
Katamani
ajiliye
Utamu kufaidia.
731
Kaamuru watumwaze
Wazanaze na wakeze
Nao
wakajitokeze
Senene kumletea.
732
Kaamuru watu wote
Ikuluni mwake mwote
Wapigwe
mvua watote
Senene kumshikia.
733
Wakampinga wahenga
Wakamba: Twahofu
janga
Utabaki bila kinga
Sote tukikuachia.
734
Akasema bila hofu
Enyi viumbe dhaifu
Mukama
ni mtukufu
Siye mfungwa sikia!
735
Hahitaji asikari
Daima kumsetiri
Kama kwamba
yu kauri
Wezi watamvamia.
736
Semeni yu wapi mtu
Ambaye angethubutu
Kuja
Ikuluni mwetu
Mukama kushambulia?
737
Nendeni enyi wavivu
Toa hapa upumbavu
Lete
senene wabivu
Ninataka kujilia.
738
Senene waliofana
Wa matumbo yalotuna
Na
vichwa vilivyonona
Ndio ninahitajia.
739
Bali si yenu maneno
Na rangi ya yenu
meno
Nendeni kwenye mavuno
Wazee mlopumbaa!
740
Wakaondoka wahenga
Nyuso zimejiviringa
Kuona
kawasimanga
Bwana wao kawashua.
741
Katika tufani kali
Manyunyu yenye ukali
Vipara
vikahimili
Senene kufuatia.
742
Mukama kabaki hali
Na vijakazi wawili
Vikongwe viso
amali
Vyangojea kujifia.
743
Na radi zikapasuka
Dhoruba ikacharuka
Na
mvua ikaanguka
Nchi ikaogelea!
744
Nchi ikazamiana
Watu wakaloweana
Senene
wafurikana
Kama nyasi wakajaa!
745
Na mvua ikawa mvua
Tufani ikazidia
Radi
zikajilipua
Na mbingu zikaungua!
746
Kama panga la maud
Umeme wafuma nti
Na
kufyeka katikati
Anga lote kwa sawia!
747
Na senene wajibwaga
Mabwawani na kuoga
Tayari
kufanywa mboga
Watu kuwatowelea.
748
Watavunjwa zao mbawa
Na miguu kung'olewa
Na pembe
kuchopolewa
Na hawatajitetea.
749
Watakongolewa wengi
Watiwe kwenye mitungi
Na
kuchemshwa kwa wingi
Hadi wamejiivia.
750
Wengine watabugiwa
Chunguni wakitolewa
Na wengine
watatiwa
Moshini kukaukia.
751
Wakazidia senene
Wanono wenye unene
Kutimia saa
nne
Bado tu wanatokea!
752
Na watu wakawapata
Kwa wingi wakawachota
Mihi yote
ikaputa
Ikajaa kuzidia.
753
Na kila mtu Kanyigo
Mkubwa hata mdogo
Alikusanya
mzigo
Wa senene kujilia.
754
Na bado walendelea
Senene kuzoazoa
Furusa
wakitambua
Haiwezi kurejea.
755
Hata Mutalala naye
Bila kujali haliye
Alichukua
fimboye
Tufanini kuingia.
756
Akichupa kama chura
Kitumboche chamkera
Senene
kiteka nyara
Aliowafumania.
757
Aliwashika mikia
Meno wasije mtia
Wakimuuma
hulia
Kisha akawaachia.
758
Hatima aliwashinda
Vichwa alipowaponda
Akaweza
kuyapinda
Meno yao ya udhia.
759
Watu wote kijijini
Walitoka majumbani
Hapakubakia
ndani
Ila waliougua.
760
Ila waliougua
Na wachache mashujaa
Ambao
walibakia
Mipango kujipangia.
761
Wakitengeza mipango
Ya kuingia ulingo
Kwa mikuki na
magongo
Himaya kujitwalia.
762
Siku hii waliona
Kaileta Maulana
Kuwawezesha
kukana
Wanaowasujudia.
763
Imeletwa na Mizimu
Kuwafanya mahakimu
Juu ya hii
kaumu
Isiyo na mtetea.
764
Hivyo walitafakari
Kwa hamu tena kwa
siri
Vipi wapate fahari
Ile waliyoijia.
765
Na wakisha kuamua
Silaha walichukua
Na kutoka
kishujaa
Kigarama kwelekea.
766
Na mvua ilifuliza
Manyunyu kuyanyunyiza
Na pepo
zilipuliza
Kwa shari ya kuzidia.
767
Senene wakianguka
Tokajuu kwa Mahoka
Juu, chini,
wafurika
Mawindo ya kujiua.
768
Walikwenda kwa harara
Bila hata
kudorora
Waenda kujipa kura
Kwa mikuki na jambia.
769
Senene walifuata
Nyuma yao kuwaita
Waende
kuwakamata
Wao hawakusikia.
770
Manyunyu yakiwatosa
Pepo zikiwapapasa
Senene
wakiwagusa
Wao wanaendelea.
771
Watu wakiwatazama
Huwafikiria wema
Hawa
wawinda wa nyama
Senene wafuatia.
772
Nao wakasonga mbele
Bila kujali kelele
Ambazo
ziwazingile
Za dhoruba na ghasia.
773
Walikwenda kwa shauku
Kwanyoyoza dukuduku
Kukabili
lao juku
Walilojiamulia.
774
Mavazi yalilowana
Baridi iliwabana
Upepo
uliwakuna
Bila wao kutambua.
775
Wakaenda, wakaenda
Kilima wakakipanda
Bila taabu na
shida
Ikulu wakelemea.
776
Hapo njia ili pweke
Walikuwa wao peke
Raia
wasioneke
Senene wajishikia.
777
Na radi zinarindima
Na dhoruba inavuma
Na baridi
imeuma
Na inamwagika mvua.
778
Bali hawa wasijali
Waenda kwa nyoyo kali
Na nyuso
zenye uvuli
Wa tamaa ya kuua.
779
Walipofika langoni
Langoni pa sulutani
Wakaingilia
ndani
Wawili si kuzidia.
780
Nyakiru aliingia
Na Kanyamaishwa pia
Na kumi si
kupungua
Langoni wakabakia.
781
Wakajiendea ndani
Na tazama sulutani
Yupo pale
sebuleni
Salama kajikalia.
782
Katika enzi kazama
Ametarama kikama
Buni
kavu anauma
Kwa raha ametulia.
783
Kakaa kama chuguu
Katulia kama nguu
Mikono hadi
miguu
Vikuku amevalia.
784
Tumbole laning'inia
Ja boga lilokomaa
Ungedhani
malikia
Ataka kujifungua.
785
Na vijakazi viwili
Vikongwe roho na mwili
Mukama
vimekabili
Bwabwaja vyambwatia.
786
Akiwaona vijana
Sulutani akanena
Karibuni
wangu wana
Ili tupate ongea.
787
Nimechoka na ukiwa
Kinywa
sijakifunguwa
Vijakazi wangu hawa
Hawajui kuongea.
788
Na wala siwalaumu
Ukabwela nao sumu
Wangakuwa
na adhamu
Kusema wangalijua.
789
Na maajuza kunena
Vilevile siyo
sana
Meno vinywani hawana
Ni fizi zimebakia.
790
Ni mkiwa mtawala
Anapokaa mahala
Patovu pa
kabaila
Wawezao kuongea.
791
Hivyo ninyi karibuni
Ijapo mu watu
duni
Kujalisi ninadhani
Mwaweza kujaribia.
792
Na mmoja mjakazi
Macho yake machunguzi
Aliyakodoa
wazi
Kwake Kanyamaishua.
793
Kwake macho alikaza
Bila kope kupepeza
Kana kwamba
anawaza
Huyu wapi katokea.
794
Akatamka Nyakiru
Ni mwema wako udhuru
Nasi
tunakushukuru
Udhuru kuutongoa.
795
Bali sisi e dubwana
Hatuji kwa
kupatana
Bali twaja kwa hiana
Mauti tumechukua!
796
Vijakazi kusikia
Vilio wakaangua
Mmoja macho
katia
Kwake Kanyamaishua.
797
Na Mukama akakaa
Amepigwa na butaa
Sauti
hakuitoa
Macho aliwakazia.
798
Nyakiru akaongeza
Hatuji
kukutukuza
Tunakuja kukukuza
Enziyo kukuambua.
799
Tunakuja kwa kisasi
Tunakuja kwa maasi
Ili
kutakasa nsi
Ambayo umechafua.
800
Twaja kukupatiliza
Kwa nguvu zake
Muweza
Ukiona unaweza
Waweza kujiokoa!
801
Na hapo Mukama Ntumwa
Tumbo akanza
kuumwa
Mbwa! Wana wa watumwa
Akili zimewapaa!
802
Akili zimewapaa
Bila nyinyi kuelewa
Mwanena
msichojua
Mwaja moto kuchezea!
803
Watoto mnazo ndwele
Bongonimwenu
zitele
Kuthubutu kama vile
Mukama kumtishia!
804
Ntumwa katu si kabwela
Ntumwamtu
kabaila
Kuguswa na mtu fala
Hilo halitatokea!
805
Mngali wana wachanga
Mmezidiwa ujinga
Akili
imewachenga
Nadhari imepungua.
806
Angalia, angalia
Kuwaonya narudia
Haliwezi
kutokea
Mnalolidhamiria!
807
Nyakiru akatongowa
Litatokea na
kuwa!
Na papo akainuwa
Mkuki na kumtia!
808
Akamfuma mkuki
Ukaingia kwa maki
Mambo
yakawa mkiki
Mukama kamrukia!
809
Kanyamaishwa tazama
Naye pia kamfuma
Mkuki
ukamzama
Na Ntumwa akaugua.
810
Akajiuma vidole
Na kupaaza kelele
Ninakufa
wangu ole
Vitwana vimeniua!
811
Na Ntumwa akageuka
Kitamtn kimetoboka
Damu
zampukutika
Akataka kukimbia.
812
Asiweze kaanguka
Hali amefadhaika
Macho
yamemkodoka
Adui yamwangalia.
813
Macho akayakodoa
Kwake Kanyamaishua
Kisha
akayashushia
Shingoni pake sikia.
814
Palepale kayakaza
Wala hakuyapepeza
Hirizi
aichunguza
Kwani ameitambua!
815
Hirizi ni ya ukoo
Mwana wake siku hio
Walipomtoa
kwao
Ali amejivalia.
816
Zamani hirizi hiyo
Mwanawe katupwa nayo
Na sasa
karudi nayo
Ni leo ayangalia.

Taswira
817
Na hili alipoona
Kajua huyu ni mwana
Mwana wake wa
laana
Kashiriki kumuua!
818
Kamba kwa sauti chungu
Enyi vijakazi
wangu
Elezeni ulimwengu
Mwanangu ameniua!
819
Na hapo akaanguka
Rohoye ikamtoka
Machoye
yakafumbika
Na shingo likalegea.
820
Nao vijakazi hao
Wakatoka mbio mbio
Wakalia
Yoo! Yoo!
Mukama wamemuua!
821
Na wale wakaingia
Nje waliobakia
Wakakuta
analia
Kanyamaishwa sikia.
822
Kanyamaishwa kasema
Moyo wangu una
homa
Sikutenda jambo jema
Mtima waniambia.
823
Maneno nimesikia
Hayati akitongoa
Ati mwana
kamuua
Mwana aliyemzaa!
824
Babangu simfahamu
Mamangu simfahamu
Walakini
nafahamu
Kiziba nilitokea.
825
Na hii hirizi yangu
Tangu utotoni
mwangu
Havaa shingoni mwangu
Sijapata kuitoa.
826
Na mama alinambia
Yule aliyenilea
'Hirizi
uliyovaa
Si ya kabwela tambua!'
827
Nikitazama usoni
Mwake huyu sulutani
Ninaanza
kuamini
Yale niliyoambiwa.
828
Nimekufuru hakika
Nimekosea Mahoka
O!
Niliyelaanika
Sisitahili afua!
829
Nyakiiru kampoza
Kaka wacha
kujisoza
Vipi kosa lakuliza
Usilolikusudia?
830
Na wala huna hakika
Kwamba aliyotamka
Mfu
yamethibitika
Ni kweli mia kwa mia.
831
Tulia tutauliza
Wazee na maajuza
Mambo yote
kueleza
Kabula ya kuamua.
832
Mengl tumesha yatenda
Kukoma hapa ni
shida
Tutafululiza kwenda
Hadi mwisho kufikia.
833
Na vijana kawambia
Maiti kumuinua
Waende
kumfukia
Kaburini kumtia.
834
Ndivyo alivyofariki
Huyu dhalimu wa
haki
Akilia kwenye dhiki
Hana wa kumtetea.
835
Ndivyo alivyofanki
Akaiacha miliki
Akaacha
halaiki
Aliyoiatamia.
836
Ndivyo alivyofariki
Akenda bila rafiki
Kwenenda
akadiriki
Kusiko na kurejea.
837
Nayo mvua ikanyesha
Na umeme ukawasha
Dhoruba
ikajirusha
Kwa nguvu za kuzidia!
838
Na Nyakiru akasema
Siwezi kuwa Mukama
Na
kuutawala umma
Peke yangu nakwambia.
839
Kanyamaishwa sikiza
Acha sasa kujiliza
Kitini
ninakukweza
Sote tutakikalia.
840
Kanyamaishwa kakana
Akasema Haja
sina
Sitayakubali tena
Ambayo wanipangia.
841
Wakabishana kwa nguvu
Saud zikawa kavu
Kila mmoja
mvivu
Ufumbuzi kufikia.
842
Nyakiru kasisitiza
Mwenzie kubembeleza
Mpenzi
nakueleza
Vema kiti kukalia.
843
Tumesafiri pamoja
Tumeteseka pamoja
Na tumeua
pamoja
Vipi sasa wanachia?
844
Tutakalia kwa zamu
Hiki kid cha adhamu
Sote
tuwe mahakimu
Watawala wa raia!
845
Mwishowe bila kutaka
Mwenzie akaitika
Ukafikiwa
mwafaka
Wote Bakama wakawa.
846
Kanyamaishwa lakini
Hakutulia moyoni
Mateseko na
huzuni
Rohoni vilibakia.
847
Na habari zikafika
Huko nje kwenye
nyika
Mukama kesha ondoka
Mambo yamesha timia!
848
Watu wote wakatoka
Nyikani wamejitwika
Senene
walioshika
Makuu kujionea.
849
Walipofika tazama
Nyakiiru ni Mukama
Na
Kanyamaishwa mwema
Kandoye kajikalia.
850
Nyumao wamejikita
Asikari wa matata
Silaha
zametameta
Kivita wamekalia.
851
Wenyeji wakauliza
Ewe mgeni eleza
Nani
amekutawaza
Ukama kukupatia?
852
Nyakiiru kaeleza
Watukufu sikiliza
Sisi
tumejitokeza
Haki zenu kutetea.
853
Tumeiona dhuluma
Aliyotenda
Mukama
Tukashikwa na huruma
Ndipo tulipomuua.
854
Mwaweza kutuhukumu
Bali hili lifahamu
Hatuji
kuwadhulumu
Tujile kuwakomboa.
855
Kama baya tumetenda
Kwa nyoka kichwa
kuponda
Mnaweza kutukinda
Kwani tu wenye hatia.
856
Chukueni misu yenu
Noeni mikuki
yenu
Sisi tu halali zenu
Mnaweza kutuua.
857
Akimaliza Nyakiru
Kuwaeleza udhuru
Raia
wakashukuru
Shangwe wakampigia.
858
Bila kufanya udhia
Wakasujudu raia
Nyakiru
wakamwambia
Nchi umeiokoa.

Taswira
859
Na wote makabaila
Wakichelea
madhila
Wakondoka halahala
Bugandika kwelemea.
860
Huko wakajikusanya
Tayari vita kufanya
Wageni
kuwanyang'anya
Enzi waliyochukua.
861
Nyakiiru akatoka
Na jeshi lilopanuka
Akaenda
Bugandika
Adui kushambulia.
862
Majeshi yakakutana
Ikawa
bimbirishana
Wakatana, wauana
Maid zikazagaa.
863
Maid zalaliana
Damu zafurikiana
Waume
wanapambana
Wengine waangamia.

Taswira
864
Na ikifika jioni
Ikadhihiri yakini
Maadui wako
chini
Nguvu zimewaishia.
865
Vitani wakajitoa
Na kuanza kukimbia
Hima
wakafuatiwa
Wengi wakaangamia.
866
Hapo vita vikakoma
Naye Nyakiru Mukama
Akarudi
Kigarama
Mukama kampokea.
867
Na pamoja kwa sawia
Kiti wakakikalia
Watu
wakasujudia
Na kuwatii kwa nia.
868
Na wakaitwa wazee
Waje wawaelezee
Ili siri
waijue
Yake Kanyamaishua.
869
Na wakiisha tamka
Ikawa hakuna shaka
Mambo
yakadhihirika
Jinsi walivyodhania.
870
Kanyamaishwa kalia
Na matanga kukalia
Babaye
kukumbukia
Na tendole kutubia.
871
Na matanga yakapita
Kanyamaishwa kapata
Maradhi
yenye matata
Asiweze kujinua.
872
Nyakiru akasumbuka
Daima ashughulika
Waganga
akiwasaka
Mwenzie kumtibia.
873
Mwisho kaona kijana
Dawa hazina maana
Sahibu
azidi sana
Mwilini kudidimia.
874
Na muda ulipopita
Mauti yakamuita
Kifo
kikamkamata
Mgonjwa akajifia.
875
Akafa Kanyamaishwa
Kakoma kutaabishwa
Shimoni
kateremshwa
Watu wakamlilia.
876
Ndivyo alivyofariki
Huyu kijana wa dhiki
Bila
kuacha kisiki
Katika hii dunia.
877
Nyakiru kamlilia
Akalia,
akalia
Akamuombolezea
Mwenzi aliyemfaa.
878
Myezi miwili Nyakiru
Katu hakuona nuru
Kijiji
hakukizuru
Nyumbani alitulia.
879
Nyumbani alitulia
Matanga kumkalia
Rafikiye wa
dunia
Ambaye hatarejea.
880
Na matanga yakiisha
Nyakiru akajikosha
Nyumbani
kajiondoshi
Nuru kuiangalia.
881
Akabaki peke yake
Mtawalaji mpweke
Akawa Mukama
peke
Kiziba kuangalia.

Taswira
882
Kisha akajenga nyumba
Akaikata na vyumba
Halafu
akaipamba
Mapambo ya kuvutia.
883
Akamaliza ujenzi
Akaleta Kachwankizi
Kaiingiza kwa
enzi
Iketi na kulowea.
884
Ndoto ikakamilika
Kachwankizi ikatika
Di! di! di!
di! kutamka
Enzi mpya kwa raia.
885
Na mjumbe akatoka
Kibumbiro akafika
Moto mpya
akateka
Kiziba akarejea.
886
Huu moto wa ukama
Uliwashwa kwa heshima
Ngoma
ilipochutama
Usiachwe kuzimia.
887
Mambo yalipotuliya
Nyakiru wakamtiya
Jina la Kibi -
Kibaya
Kwani watu ameua.
888
Akalikubali jina
Kwa moyo wa kiungwana
Na ndivyo
ajulikana
Katika historia.

Taswira
889
Hapa sasa nakomea
Kituo nimefikia
Nyuma
yaliyotokea
Hapa sitasimulia.
890
Nimesema ya kutosha
Na wala sikupotosha
Na hadithi
imekwisha
Tamati tumefikia.
891
Mtunzi ni chipukizi
Mugyabuso Mulokozi
Mulokozi ni
mzazi
Baba aliyemzaa.
892
Ni kijana atokea
Upeo hajafikia
Makosa
ukimtoa
Sana
atafurahia.