Cover Image
close this bookUtangulizi wa Lugha na Isimu (Tanzania Publishing House Dar Es Salam, 1994, 121 p.)
View the document(introduction...)
View the documentShukurani
Open this folder and view contentsSura ya Kwanza: Ujuzi wa Lugha
Open this folder and view contentsSura ya Pili: Fonetiki: Sauti za Lugha
Open this folder and view contentsSura ya Tatu: Fonolojia: Mfumo-sauti wa Lugha
Open this folder and view contentsSura ya Nne: Mofolojia: Muundo wa Maneno
Open this folder and view contentsSura Ya Tano: Sintakisia: Muundo Wa Sentensi
View the documentKinyume

Shukurani

Kitabu hiki kilianzwa kuandikwa nilipokuwa kwenye likizo ya masomo katika Idara ya Lugha na Isimu, Chuo Kikuu cha York, Uingereza (Oktoba 1987-Juni 1988). Nilikamilisha kukiandika nilipokuwa katika Taasisi ya Mafunzo ya Lugha na Utamaduni wa Asia na Afrika, Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Kigeni cha Tokyo, Japan (Oktoba 1992-Septemba 1993). Natoa Shukurani zangu za dhati kwa Taasisi zote mbili kwa kunipatia nafasi nzuri ya kutulia na kuweka mawazo yangu pamoja.

Wanafunzi wangu wa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, toka nilipoanza kufundisha mwaka wa 1972, wamenipa moyo wa kuandika kitabu hiki. Isimu ni somo la nadharia, na kulifundisha katika Kiswahili bila kitabu cba kiada kilichoandikwa katika lugha hii, ilikuwa mzigo mzito kwa wanafunzi na kwa walimu pia.

Walimu wenzangu wa Idara ya Kiswahili nawashukuru kwa kuchangia mawazo yao katika somo hili la isimu.

Shukurani zangu nyingi napenda kuzitoa kwa Profesa D. J. Mkude wa Idara ya Kiswahili ambaye, pamoja na shughuli zake nyingi za Utawala, alikubali kusoma mswada wote wa kitabu hiki na kunipa maoni ambayo yalisaidia sana kuurekebisha mswada huu. Lakini hahusiki na kasoro zozote zitakazoonekana katika kitabu hiki!

Mwisho, napenda kuwashukuru wanangu, Kighenda Tiginihate, Wende Nkomboa, na Nesiya Neema Tumalile, kwa upendo na uvumilivu wao, na hasa walivyokubali kuishi nami katika nchi za kigeni bila kulalamika.