Cover Image
close this bookUchambuzi na Uhakiki - Fungate ya Uhuru (Dar Es Salaam University Press, 1991, 19 p.)
View the document(introduction...)
View the document1. Miongozo ya Lugha na Fasihi
View the document2. Namna ya Kuitumia
View the document3. Mwandishi
View the document4. Maana ya Fungate
View the document5. Uwiano Wake na Dhana ya Uhuru
Open this folder and view contents6. Dhamira Kuu
View the document7. Falsafa ya Fungate ya Uhuru
Open this folder and view contents8. Fani ya Fungate ya Uhuru
View the document9. Maswali

1. Miongozo ya Lugha na Fasihi

MIONGOZO ya Lugha na Fasihi ni mfululizo uliokusudiwa wanafunzi na wapenzi wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Mfululizo huu umebuniwa kutokana na lengo la kuwasaidia wanat’unzi wa lugha na fasihi katika ngazi mbalimhali za taaluma zao, hasa wale wanaojiandaa kwa mitihani ya Taifa. Mtululizo huu utatoa vijitabu ambavyo vitakuwa vinasaidia kuchambua vitabu vya lugha, na fasihi ambavyo vimeteuliwa na Wizara ya Elimu vitumike kuwatahini wanafunzi katika vyuo na sekondari nchini. Kwa hali hiyo, mfululizo huu utajumuisha uchambuzi wa vitabu vilivyochapishwa na Dar cs Salaam University Press (DUP) na vile ambavyo vitakuwa vimechapishwa na mashirika mengine.

Uchambuzi wa kila kitabu utazingatia fani na maudhui yanayojitokeza katika kazi hiyo, na mwishoni kuna maswali ambayo yanamwongoza mwanafunzi. Miongozo hii imeandaliwa kwa kuzingatia utaalamu wa hali ya juu ili kurahisisha usomaji wa kitabu kinachohusika. Wanafunzi na wapenzi wa lugha na fasihi watafaidika mno na mfululizo huu. Mhariri mwanzilishi wa mfululizo huu anawatakia usomaji mwema.