Cover Image
close this bookUchambuzi na Uhakiki - Fungate ya Uhuru (Dar Es Salaam University Press, 1991, 19 p.)
View the document(introduction...)
View the document1. Miongozo ya Lugha na Fasihi
View the document2. Namna ya Kuitumia
View the document3. Mwandishi
View the document4. Maana ya Fungate
View the document5. Uwiano Wake na Dhana ya Uhuru
Open this folder and view contents6. Dhamira Kuu
View the document7. Falsafa ya Fungate ya Uhuru
Open this folder and view contents8. Fani ya Fungate ya Uhuru
View the document9. Maswali

7. Falsafa ya Fungate ya Uhuru

Diwani ya Fungate ya Uhuru inatetea itikadi ya Ujamaa. Itikadi hii ina mashiko makubwa miongoni mwa Watanzania wengi - kuanzia wasanii na hata watu wa kawaida. Khatib ni mtetezi wa Ujamaa. Anakemea na kulaani wizi, dhuluma na majivuno ya kirasimu.

Kiuongozi, Khatib angependa nchi ya Tanzania iongozwe kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa. Lakini pia haielekei kuonyeshwa kwamba mambo haya si rahisi sana kuonekana miongoni mwa jamii - hasa katika nchi ya chama kimoja cha kisiasa.

Hata hivyo, katika mazingira mengine, tunamwona mshairi angependa kusema mambo mbalimbali, lakini yaelekea hana uhuru. Hali hii inajitokeza katika shairi lake la “Nataka Kusema” (uk. 14).

Kwa kuzingatia nafasi aliyonayo katika serikali ya Tanzania, Khatib ana uhuru mdogo sana wa kusema. Kwa huzuni, mwandishi anaeleza nia yake:

Nataka, kusema yote,
YOTE, yaniumizayo MOYO, lakini;
Nna kitata, siwezi kutamka!

...

Nataka, kulia kite,
KITE, yanikeketayo MOYO, lakini
Hayatatokea, machozi, yametweka!

...

...wenzangu,
Wamepofuka, viziwi, na mabubu!

Khatib hana uhuru wa kusema ingawa angependa kusema.

Khatib pia anaelekea kutetea maadili bora katika jamu na pia mapenzi ya dhati. Hii aghalabu si falsafa mpya kwa mwandishi huyo, kwani inajitokeza pia katika vitabu vyake vya Pambazuko la Afrika, Utenzi wa Ukombozi wa Zamibar, na diwani hii ya Fungate ya Uhuru.