Cover Image
close this bookKamusi ya Istilahi za Sayansi na Tekinolojia (BAKITA - UNICEF, 1992, 44 p.)
View the document(introduction...)
View the documentUtangulizi
View the documentMaelezo kwa Mtumiaji
View the documentFani ya Sayansi
View the documentFani ya Sayansi Kimu
View the documentFani ya Ufinyanzinakshi, Mkonge, Mianzi na Vibuyu
View the documentFani ya Ufundi
View the documentFani ya Ufundi Viatu
View the documentFani ya Usindikaji Mafuta na Matunda, na Utengenezaji wa Sabuni
View the documentFani ya Utengenezaji wa Karatasi, Matofali na Vigae
View the documentKinyume

Fani ya Utengenezaji wa Karatasi, Matofali na Vigae

Aa

alumini ji aluminium: metali nyeupe laini na nyepesi ambayo hutumika kutengeneza nyaya za umeme, mabomba na mabati.

alumu ji sulphate: msombo ambao hufanya vitu vihimili moto.

alamu ya alumini ji aluminium sulphate: msombo ambao hutumiwa kutuliza nyuzinyuzi za karatasi na kuongeza ugumu wake.

Bb

bakuli ji trough: chombo mfano wa hori kinachotumiwa kwa kupondea vitu.


bakuli

bapa kv flat: -enye uso uliosawazika.

buluu ji blue: taz. buluu: MIANZI, MKONGE, UFINYANZINAKSHI NA MABUYU.

Cc

chumba cha kukaushia ji drying chamber: sehemu ndani ya jengo yenye joto inayotumika kuwekea vitu vyenye majimaji ili viwe vikavu.

Dd

dai ji dye: kioevu kinachotumika kukipa kitu kingine (kama karatasi, ngozi, nguo, n.k.) rangi.

dai asilia ji natural dye: rangi awali inayopata kitu kabla ya kupata rangi nyingine.

dhibiti ubora kt control quality: kuhakikisha kuwa ubora wa bidhaa unabakia katika kiwango chake au kuwa bora zaidi.

diako ji diacol: kemikali ambayo huzifanya chembechembe za karatasi (grains) zijipange vizuri na zishikane.

dohani ji chimney: bomba maalumu la kutolea moshi nje ya tanuri au jiko.

dutu ji substance: kitu chochote chenye mata.

Ee

eneo la kinu karatasi ji effective area of paper making: mahali au sehemu ambapo mchakato wa kutengeneza karatasi hufanyika.


dohani

fueli ji fuel: dutu yoyote inayochomwa kuwa chanzo cha joto au nguvu, k.m., makaamawe au petroli.

funjo ji papyrus: mmea wenye majani yanayofanana na nyasi ambao huota kwenye sehemu za majimaji na hutumika kutengeneza karatasi.

fyatua kt mould: tengeneza tofali kwa kutumia kibao maalum.

Gg

gome ji bark sehemu ngumu ya nje ya mti, au pengine huitwa gamba.

Kk

kalibu ji mould: kifaa kinachoyapatia umbo maunzi yanayomiminwa ndani yake.

kalibu karatasi ji paper mould: mashine au kifaa cha kuweka tetefya ya karatasi ili ipate umbo maalum.

kamua kt press: minya kitu ili kutoa maji, k.m., kukamua karatasi rojorojo.

kapi ji pulley: kifaa duara chenye mfuo kukizunguka.

kapi bapa ji flat pulley: roda isiyo na nafuo mbinuko.

kemikali ji chemical: dutu inayotumika au kutengenezwa katika kemia.

kiawiza maji ji water discharger: sehemu ya kutolea maji nje.

kiawizi ji discharger: sehemu ya kutoka kitu nje, k.m., dohani.

kigae ji tile: kipande cha udongo kilichotengenezwa kutokana na udongo wa mfinyanzi na baadaye kuchomwa. Hutumiwa kuezekea nyumba.

kihero ji vat: chombo cha kuwekea tetefya ya karatasi ili baadaye ikaushwe na kuwekwa katika umbo linalotakiwa.

kipashio ji beltlace: kipande cha chuma kinachotumiwa kuunganisha ukanda.

kishikio ji anchor: kitu kinachotumiwa kushikilia kitu kilichotundikwa.

kitambaatenga ji felt: kipande cha nguo ambacho huwekwa tetefya ya karatasi wakati wa kukausha.

kivutio ji driver: kifaa kinachotumiwa kutoa kitu kingine, k.m., roda, bisibisi.

kivuvio ji hopper: kifaa ambacho hupuliza hewa ya kukaushia kitu au vitu haraka.

kiwanda ji factory: mahali ambapo vitu hutengenezwa, k.m. kiwanda cha karatasi, nguo.

kiwinga ji repellant: kitu kinachozuia kupenya kwa maji au kioevu kingine.

kiwinga maji ji water repellant: dawa ambayo hutumiwa kuzuia karatasi isinyonye maji au wino.

kuru ji roller: magurudumu yenye uwezo wa kusafirisha vitu yakirivingika.

Mm

mafutakaukia ji drying oil: mafuta ambayo ni rahisi kukauka. Hutumika kwenye wino wa kupigia chapa na rangi za mafuta.

makaamawe ji coal: madini meusi yanayotumika kama fueli.

malighafi ji raw material: vitu vitumiwavyo, aghalabu viwandani, kutengenezea bidhaa.

mashine ya kukamulia ji hydraulic press: mtambo wa kukamulia karatasi kutoa maji.

maunzi ji material: taz. maunzi: USINDIKAJI MAFUTA, MATUNDA NA UTENGENEZAJI SABUNI.

mchakato ji process: mlolongo mzima wa kufanya au kutengeneza kitu au vitu.

mfereji ji chanuel: mtaro au njia ambamo maji au vioevu vingine hupita.

mfinyanzi ji porter: mtu anayetengeneza vitu vya udongo.

mkanda ji belt: kipande kirefu cha nguo, ngozi au mpara kinachozungushwa katika oda.

mumiani ji formalydehyde: kemikali ambayo hutumika kama mputio wa kuhifadhia karatasi zisioze.

Pp

pararisha kt bleach: kufanya rangi ya kitu ififie, k.m., rangi ya nguo.

poda pararishi ji bleaching powder: ungaunga unaotumiwa kufifisha rangi ya kitu, aghalabu, nguo.

pondeo ji beater: mashine ya kumeng’enyea au kulainisha malighafi ya karatasi. Pia tetefya.

Rr

rangi ji colour: kemikali inayotiwa katika vitu vionekane tofauti na vilivyokuwa awali.

roda ji pulley: taz. kapi

rozini ji rozine: dawa inayozuia karatasi zisinyonye maji na kupunguza uzito.

Ss

sampuli ji sample: mfano halisi wa kitu.

Tt

tanuri ji kiln: jengo ambamo matofali au vigae huchomwa.

tetefi ji pulp: kitu laini kama ujiuji. Nayo tetefi ni malighali ya karatasi inayopondwapondwa na kuchanganywa na maji.

tofali ji block: bonge linalotengenezwa kwa kuchanganya saruji, mchanga na maji.

trei ji tray: chombo bapa cha kubebea vitu chenye kingo zilizoinuliwa.


trei

trei ya mali ghafi ji feeding tray: chombo bapa cha kuwekea malighafi iliyo tayari kuongezwa kwenye mashine.

Uu

umeme ji electricity: nishati inayoweza kubadilishwa kuwa nuru au joto.

Vv

vali ji valve: kifaa kinachomhusu uingiaji na utokaji wa vioevu na gesi kuelekea upande mmoja tu.