
| Tafsiri Sanifu - Toleo la 4 (Standard Translation) (BAKITA, 1998, 79 p.) |
Hili ni toleo la nne katika mfululizo wa matoleo ya TAFSIRI SANIFU ambayo la kwanza iilichapishwa mwaka 1974. Katika muda huo, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limetoa jumla ya istilahi 7,480 katika fani zifuatazo:
|
1. Bayolojia |
349 |
|
2. Biashara na Uchumi |
943 |
|
3. Bunge |
274 |
|
4. Elimu |
62 |
|
5. Fizikia |
203 |
|
6. Hisabati |
652 |
|
7. Historia |
198 |
|
8. Jiografia |
629 |
|
9. Kemia |
195 |
|
10. Maktaba na Ujalidi |
122 |
|
11. Sayansi Kimu |
1979 |
|
12. Sayansi ya Lugha |
185 |
|
13. Siasa |
243 |
|
14. Tekinolojia/Ufundi |
276 |
|
15. Uendeshaji na Uongozi |
1064 |
|
16. Urasimu (= Uchorajiwa kifundi) |
106 |
Kazi hii muhimu inaendelezwa kwa nguvu ili hatimaye ikamilike na kulifikia lengo la kukifanya Kiswahili kiwe na uwezo wa kueleza, kuaridhia na kufafanua maarifa na taaluma mbalimbali bila ya kuwa na upungufu.
TAFSIRI SANIFU Toleo la 4 ni kitabu chenye jumla ya istilahi 2,958, katika fani ya: Bayolojia, Fizikia, Historia, Jiografia, Kemia, Sayansi Kimu, Siasa, Tekinolojia (Ufundi), Uendeshaji na Uongozi, na Urasimu. TAFSIRI SANIFU ni istilahi muhimu katika taaluma nazo zimekusudiwa kukidhi haja kubwa ya istilahi za Kiswahili zinazotakiwa na wananchi katika harakati zao za kila siku. Baraza laKiswahili la Taifa (BAKITA) litaendelea kuimarisha, kudhibiti na kuifanya kazi hii iwe nzuri na bora zaidi kwa kuuzatiti uhusiano na ushirikiano uliopo baina yake na vyombo vingine vya Kiswahili na kuukuza.
Kwa niaba ya BAKITA napcnda kuipa pongezi Kamati ya Kusanifu Lugha (KAKULU) kwa juhudi kubwa inayoifanya katika kazi hii. Pia kwa niaba ya BAKITA, natoa snukrani nyingi kwa ushirikiano mzuri katika kuijadili, kuihakiki na kuiandaa kazi hii. Vyombo vinavyostahiki pongezi na shukrani kwa kutoa mchango mkubwa ni hivi vifuatavyo:-
1. Taasisi ya Elimu
2. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili - Chuo Kikuu
3. Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni - Zanzibar
4. Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
5. Idara ya Kiswahili - Chuo Kikuu
6. Idara ya Sanaa za Maonyesho - Chuo Kikuu
7. Idara ya Lugha ya Taifa - Utamaduni na Vijana
8. Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA)
9. Kamati za Kiswahili - Mikoani, Wilayani, Ofisini na Viwandani
10. Chama cha Kiswahili - Chuo Kikuu
11. Watu binafsi - Wataalamu, mabingwa na wapenzi wa Kiswahili.
Tunatarajia kuwa mambo mawili muhimu yatazingatiwa. Kwanza kwamba uhusiano na ushirikiano uliopo utaendelea kukuzwa siku baada ya siku mpaka tulifikie lengo la harakati zetu za kukikuza na kukieneza Kiswahili. Pili, tutapokea maoni na mapendekezo ya vikundi au watu binafsi hasa yanayohusu fikra za kisayansi kuhusu uendelezaji wa kazi hii ambayo ni wajibu na haki yetu sote.
Profesa G.A. Mhina
MWENYEKITI
BARAZA LA KISWAHILI LA
TAIFA
(BAKITA)