
| Ham volume 8 - Jarida la mabadiliko na uimarishaji wa sekta ya Afya Tanzania (Wizara ya Afya, 1998, 38 p.) |
HAM
|
VOLUME 8 |
NO. 3 1998 |
ISSN 0856-395 |
MADHUMUNI
Kuwasiliana na jamii kwa lengo la:
· Kuelimisha wafanyakazi wa afya wa ngazi mbalimbali pia wafanyakazi wa sekta nyingine na wananchi kwa jumla kuhusu mambo ya mabadiliko na uimarishaji wa sekta ya afya.· Kuwapa fursa wasomaji kujadili au kutoa maoni yao kuhusu mambo mbalimbali yanayoweza kusaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
· Kuwafahamisha juu ya matukio mapya katika fani ya afya.
· Kuhamasisha umma kutambua wajibu wao katika kuinua hali ya afya kwa juhudi zao wenyewe.
MAKALA
Tunapokea na kuchapisha makala, habari za matukio, picha au maoni kutoka kwa wasomaji. Tunazingatia mamboya mabadilikona uimarishajiwa huduma za afya kwa jamii. Makalahizo zinaweza kuwa juu ya mambo mbalimbali katika fani ya afya kama:-
· Utekelezaji wa mpango wa kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.
· Utekelezaji wa vipengele mbalimbali vya Huduma za Afya ya Msingi.
· Shughuli za mipango/miradi ya Wizara ya Afya.
· Maoni kuhusu muundo na uonaozi wa sekta ya afya katika ngazi mbalimbali.
· Juhudiza wananchi wenyewe katika masuala ya kuboresha afya zao.
· Mashairi na vikaragosi.
Mkazo wetu pia ni wakuandika kuhusu juhudi za kushirikisha jamii na sekta nyingine katika masuala ya kufanikisha utoaji wa Huduma ya Msingi.
USAMBAZAJI
Jarida hili husambazwa kwenye mikoa yote ya Tanzania. Njia mojawapo inayotumiwa ni usambazaji kwa kufumia utaratibu wa kupeleka masanduku ya dawa muhimu kwa kupitia Idara Kuu ya Dawa (MSD).
Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali hupatiwa nakala za jarida hili kupitia kwenye Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO).
Hospitali za Rufaa hupatiwa nakala zao moja kwa moja.
Nakala nyingine husambazwa kwenye Wizara nyingine, na Maktaba. Baadhi ya miradi inayoshughulikia huduma za Afya ya Msingi huagiza nakala nyingi (kwa kulipia) na kuzisambaza kwenye sehemu zao zinazowahusu.
|
Picha ya Jalada: | |
| | |
|
Mbele: |
Wajumbe wa mkutanowa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa uliofanyika mkoani Mtwara. |
| | |
|
Nyuma: |
Maelezo kuhusu ongezeko la idadi ya watu. |
| | |
|
MHARIRI | |
|
G. K. Mtavangu | |
| |
|
|
WAHARIRI WA MAKALA |
WASANII |
|
E. Nchimbi |
A. D. R. Samki |
|
F. Lubuva |
P. Gustav |
|
N. Jabir | |
|
T. Ndziku | |
Jarida hili hutolewa na Wizara ya Afya na Kuchapishwa na Colour Print (T) Limited.

Uongozi wa watu? Nenda taratibu,
Vunja hilo fimbo kubwa!
|
HAM: |
Jarida hili linatolewa na Wizara ya Afya, Sekretarieti ya Mpango wa Mabadiliko ya Uimarishaji wa Sekta ya Afya Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA). |