Cover Image
close this bookHam volume 8 - Jarida la mabadiliko na uimarishaji wa sekta ya Afya Tanzania (Wizara ya Afya, 1998, 38 p.)
View the document(introduction...)
View the documentViongozi wapya Wizara ya Afya
View the documentTahariri
View the documentChiduo asisitiza umuhimu wa mabadiuko ya sekta ya afya
View the documentMkutano wa waganga wakuu wa mikoa 1998
View the documentMfumo wa afya wa wilaya
View the documentChangamoto mpya kwa afya ya jamii
View the documentMfumo wa taarifa kwa ajili ya uendeshaji
View the documentMagonjwa Mapya ya kuambukiza na yanayojirudiarudia
View the documentUgonjwa wa Kisukari
View the documentMabadiliko ya idadi ya watu Tanzania
View the documentSera ya idadi ya Watu
View the documentIdadi ya Watu na Mazingira
View the documentTaarifa ya ongezeko la Wazee Duniani
View the documentMatatizo ya wazee katika jamii
View the documentUnapata uzoefu gani kutokana na maelezo ya kazi za mganga wa wilaya huyu?
View the documentJitihada za Kimataifa za kupambana na ugonjwa wa Malaria
View the documentShirika la afya duniani na mapambano dhidi ya Ukimwi
View the documentUsalama wa damu ni muhimu kudhibiti ukimwi
View the documentAthari ya Ukimwi Wilayani Makete
View the documentChangamoto za kimaadili na haki za binaadamu zinazowakabili wafanyakazi
View the documentWanawake na watoto ni sehemu muhimu katika jamii
View the documentHuduma ya Wakunga wa jadi Tanzania
View the documentAthari za Tumbaku, pombe na madawa kwa mama mjamzito
View the documentBushi
View the documentMabadiliko ya muundo wa uendeshaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
View the documentKilio cha wakimbizi na maisha ya kifamilia
View the documentWafadhili na Maskini
View the documentMatangazo
View the documentChemsha maji yako
View the documentMaadili ya PCB (Cost of Conduct)
View the documentKisa cha mtaalam wa afya kwa jamii
View the documentKinyume

Mabadiliko ya idadi ya watu Tanzania

Ongezeko la Idadi ya Watu

Idadi ya watu Tanzania iliongezeka kutoka watu milioni 7.7 mwaka 1948, ilipohesabiwa kwa mara ya kwanza, hadi watu milioni 12.3 wakati wa uhuru mwaka 1967, na kufikiawatu milioni 23.1 katikati ya mwaka 1988. Katika kipindi cha miaka 40 kutoka mwaka 1948 hadi mwaka 1988, idadi ya watu Tan-zania imeongezeka mara tatu, wakati idadi ya watu dunaiani imeongezeka mara dufu. Kwa mwaka 1993, idadi ya watu Tanzania inakadiriwa kuwa ni milioni 27, na inaongezeka kwa kiasi cha watu 750,000 kwa mwaka.


Ongezeko la Idadi ya Watu Tanzania

Chanzo cha kuongezeka kwa idadi ya watu

Mabadiliko katika idadi yawatu yanachangiwa na vitu vitatu navyo ni: watoto wanaozaliwa, idadi ya vifo vilivyotokea na idadi ya watu waliohamia na waliohama kutoka katika nchi. Kwa vile kiwango cha uhamiaji wa kimataifa ni kidogo sana hapa Tanzania, ongezeko la watu kwa kiasi kikubwa linatokana na tofauti baina ya uzazi kwa upande mmoja, na vifo kwa upande mwingine vinavyotokea kila mwaka.

Tofauti kati ya kiwango cha uzazi na kiwango cha vifo katika mwaka ni sawa na ongezeko la asili la idadi ya watu. NchiniTanzania kiwango cha ongezeko la asili kimeongezeka kutoka asilimia 2.3 mwaka 1 957 hadi kufikia zaidi ya asilimia 3.0 mwaka 1987. Kwa hiyo ongezeko letu la haraka la idadi ya watu limetokana na ukweli kwamba wakati kiwango cha vifo kimeshuka kwa kiasi kikubwa, kiwango cha uzazi kimeendelea kubaki juu. Endapo kasi ya ongezeko la watu itaendelea kwa kiwango cha sasa, idadi ya watu Tanzania itaongezeka mara dufu katika muda wa miaka 20 hadi 25 ijayo.

Shinikizo la Kuongezeka kwa idadi ya Watu

Takwimu za hivi karibuni kutokana na sensa ya mwaka 1 988 na uchunguzi wa kidemografia na kiafya ulifanyika 1991/92 vinaonyesha kwamba kiwangocha uzazi kinaweza kuwa kimeanza kushuka. Hata hivyo, jambo muhimu la kuzingatia hapa ni kwamba idadi ya watu itazidi kuongezeka kwa miaka mingi ijayo licha ya lolote litakalotokea kwa kiwango cha uzazi. Hii ni kwa sababu hivi sasa idadi kubwa ya Watanzania ni watu ambao ni wa umri chini ya miaka 15.

Hivi sasa nchini Tanzania wanawake wengi wanazaa wastani wa watoto 6.5 katika maisha yao ya uzazi. Ili idadi ya watu iache kuongezeka inabidi wastani huu upungue hadi kufikia kama watoto wawili kwa kila mwanamke. Hata hivyo, hata kama kiwango cha uzazi kimepungua kwa kiasi hicho hivi leo, bado idadi ya watu itaendelea kuongezeka kwa muda wa miaka mingi ijayo.

Hii inaweza kuelezeka kutokana na ukweli kwamba katika miaka 20 ijayo watoto wa leo watakuwa wamefikia umri wa kuzaa, na watakuwa ni wengi zaidi ya wale ambao wamemaliza muda wao kwa kuzaa. Kwa vile watu wenye uwezo wa kuzaa watakuwa wengi, hata kama kila familia wataamua kuzaa watoto wawili tu, idadi ya mazalisho itakuwa kubwa kuliko vifo, na idadi ya watu itazidi kukua. Ongezeko hili litaendelea mpaka hili kundi la watu wengi lipite, kwa muda wa - karibu miaka 40.


Matazamio ya Ukubwa wa Familia

Matazamio ya Makadirio ya Idadi ya Watu

Ijapokuwa ongezeko, la idadi ya watu ni jambo lisiloepukika, kasi ya ongezeko na kiasi cha ongezeko ni mambo ambayo yanategemea kiwango cha uzazi, vifo na uhamiaji. Ili kuweza kuona athari za ongezeko la watu hadi mwaka 2020. Makadirio haya mawili yanatofautiana tu kwa matazamio ya kiwango cha uzazi.

Kipimo kimojawapo cha kiwango cha uzazi ni wastani wa watoto ambao mwanamke anazaa katika kipindi cha maisha yake. Sensa ya mwaka 1988 ilikadiria kiwango cha uzazi kuwa ni watofo 6.5. Katika mchanganuo wetu, kuendelea kwa kuongezeka kwa haraka kwa idadi ya watu kumeonyeshwa katika kadirio “A” ambako kiwango cha uzazi kimekadiriwa kubakia 6.5 kwa muda wa miaka 30. Katika hali tofauti, kadirio “B” kiwango cha uzazi kinapungua kufikia nusu katika muda wa miaka 30 kutoka watoto 6.5 mwaka 1990 hadi 3.25 ifikapo mwaka 2020.

Haya matazamio sio makadirio ya kiwango cha uzazi kitakavyokuwa hapo baadaye, bali ni makadirio tu ya kubuni ambayo yatatuwezesha kuona athari za kiwango cha chini cha uzazi kwa hapo mbeleni.

Matazamio ya kiwango cha vifo ni sawa katika hali zote mbili, na yanaonyeshwa kwa wastani wa umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa. Katika hali zote mbili wastani wa umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa unatazamiwa kuongezeka kutoka miaka 47 ya sasa kwa wanaume na 55 kwa wanawake ifikapo mwaka 2020. Matazamio haya, ambayo yanatokana na takwimu za hivi karibuni pamoja na mashauriano ya wataalam wa Tan-zania, kwa kiasi fulani ni ya chini kuliko yale yalivyotumiwa na makadirio yaliyofanywa huko nyuma na shirika la Umoja wa Mataifa (UN) na Benki ya Dunia. Endapo kiwango cha vifo kitateremka kwa kiwango kuliko inavyodhaniwa hapa na kufanya wastani wa umri wa kuishi uongezeke, matokeo yakeyangekuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuliko inavyoonekana hapa.

Mfano huu vile vile umetilia maanani athari za UKIMWI katika ongezeko la idadi ya watu. Japokuwa ni vigumu sana kutabiri ugonjwa huu utaendelea kwa kiasi gani hapo mbeleni, tunatazamia kwamba UKIMWI, utaendelea kuenea miongoni mwa watu wazima kwa kiwango cha asilimia 6.5 mpaka 10 katika miaka 10 ijayo. Katika hali hii, kwa hali zote mbili “A” na “B”, idadi ya watu inavyokadiriwa kwa mwaka 2020 ni ndogo kwa asilimia 10 kuliko ambavyo ingekuwa endapo kuenea kwa UKIMWI kungesimama leo hii.

Wingi wa watu

Kwa kutumia matazamio ya hapo juu, mfano huu unatoa idadi ya itakavyokuwa hapo mbeleni kwa Tanzania nzima, Bara naVisiwani.

Endapo kiwango cha uzazi kitaendelea kuwa juu, idadi ya watu ya mwaka 1990 ya watu milioni 24.6 itaongezeka zaidi ya mara dufu na kufikia watu milioni 58 ifikapo mwaka 2020. Endapo kiwango cha uzazi kitapungua, bado idadi ya watu itaongezeka kwa kiasi cha kutosha katika kipindi cha miaka 30 ijayo na kufikia watu milioni 44 mwaka 2020. Hata hivyo, idadi hii ni pungufu kwa asilimia 25% ukilingamisha na hali ambayo ingekuwa endapo kiwango cha uzazi kingebakia juu kama ilivyo sasa. Tofauti hii ya idadi ya watu katika hali hizi mbili watu milioni 14 ni matokeo ya kupunguza kiwango cha uzazi.

Katika sura zifuatazo tunatazama athari za hali hizi mbili za ongezeko la watu kwa uchumi, afya, elimu, mazingira na ukuaji wa miji.


Idadi ya Watu