
| Ham volume 8 - Jarida la mabadiliko na uimarishaji wa sekta ya Afya Tanzania (Wizara ya Afya, 1998, 38 p.) |
Msingi unaoongoza Sera ya idadi ya watu hapa Tanzania ni kwamba idadi ya watu na maendeleo ni sura mbili za sarafu moja, mambo yote mawili lazima yashabihiane na yaunganishwe. Kwa hali hiyo, lengo kuu la sera ya idadi ya watu ni kuimarisha maendeleo ya Taifa.
Malengo mahsusi ni:-
· Kuingiza kwa kikamilifu vipengele vya idadi ya watu katika mipango ya kiuchumi kwa njia ya kutoa, kusambaza na kutumia takwimu za masuala ya idadi ya watu na maendeleo.· Kufikia kasi ndogo ya o ngezeko la idadi ya watu kwa kupunguza kiwango cha uzazi kwa kila mtu kwa kuamua mwenyewe;
· Kuimarisha afya ya jamii kwa ujumla pamoja na makundi ambayoyanakabiliwa na hatari kubwa yaani wanawake na watoto, kwa kupunguza vifo na magonjwa;
· Kuleta uwiano mzuri wa kimaendeleo kati ya vijiji, miji na mikoa, ili kuwa na mtawanyiko mzuri zaidi wa idadi ya watu kwa matumizi bora ya rasilimali za Tanzania;
· Kuleta usawa katika haki, nafasi za kati na maisha kwa wananchi wote na mkazo zaidi ukiwa katika kuinua hadhi ya wanawake;
Mpango madhubuti wa utekelezaji utafuata mbinu zifuatazo:-
· Kuongeza uwezowa kuingiza vipengele vya idadi ya watu katika mipango ya maendeleo;· Kuanzisha mpango madhubuti wa habari, elimu na mawasili-ano;
· Kuhakikisha kushirikishwa kwa wanawake katika shughuli zote za program;
· Kuendeleza program za watoto, vijana na wazee;
· Kuimarisha program za kilimo na chakula, pamoja na lishe, na kuendeleza hifadhi za mali ya asili.
Sababu Zinazochangia Kiwango Kikubwa cha Uzazi
Katika Tanzania kuna sababu mbili kubwa zinazochangia kuwa na kiwango kikubwa cha uzazi. Ya kwanza, ni kwamba wanawake wanaolewa wakiwa na umri mdogo, na karibu wanawake wote wanaolewa. Katika kukabiliana na jambo hili, sera ya taifa ya Idadi ya Watu inapendekeza:-
· Kupunguza kiasi cha wanawake wanaolewa kabla ya ya kufikia umri wa miaka 20 kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2000;· Kuinua hadhi ya mwanamke;
· Kuendeleza elimu baada ya elimu ya msingi kwa wanawake na wanaume;
· Kuongeza nafasi za ajira kwa wanawake;
· Kubadilisha sheria za ndoa, familia, mgawanyowa mali na ajira ambazo zinabagua kwa misingi ya kijinsia
Sababu ya piii kubwa inayochangia kwa kiwango kikubwa cha uzazi ni kutokuwepo kwa mipango mizuri ya uzazi katika ndoa. Malengoya sera kwa ajili ya kurekebisha jambo hili ni pamoja na:-
· Kila familia izae watoto wanaopishana kwa muda wa miaka miwili (2);· Kuelekeza program za elimu ya maisha ya familia na huduma za uzazi wa mpango kwa wanaume na wanawake;
· Kufanya huduma za uzazi wa mpango ziweze kupatikana kwa watu wote wanaozihitaji.
Faida ya mpango mzuri wa kupunguza kasi ya ongezeko la watu.
Maendeleo ya haraka na ya kudumu ya kujamii na uchumi yatahitaji sera nzuri zinazoleta kukua kwa rasilimali ya binaadamu pamoja na uwezowa kiuchumi. Mchanganuo huu unaonyesha athari za ongezeko la watu kwa malengoya kiujumla ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kama tulivyoona, mpango mzuri wa kupunguza kasi ya ongezeko la watu utasaidia juhudi za:-
· Kukuza uchumi na kuongeza wastani wa pato la kila mtu,· Kupunguza mzigo kwa wale wenye uwezo wa kufanya kazi na kuongeza nafasi mpya za kutosha za ajira,
· Kutoa huduma bora za afya kwa watu wote,
· Kuboresha afya na maisha ya kina mama na watoto,
· Kufikia na kudumisha kiwango kizuri cha elimu,
· Kuwa na utarafibu mzuri wakujitosheleza chakula muda wote,
· Kuhifadhi misitu yetu na kudumisha viwango vya matumizi vinavyohakikisha kuendelea kuwepo kwa rasili-mali ya kutosha,
· Kuhakikisha huduma za kutosha, ikiwa ni pamoja na nyumba za kuishi vinapatikana kwa ajili ya watu wa mijini wanaozidi kuongezeka.