Cover Image
close this bookMafunzo ya ng'ombe kuwa Maksai na matunzo yake (Wizara ya Kilimo na Ushrika, 1997, 19 p.)
close this folderSura ya tatu
View the documentMatunzo ya Maksai

Matunzo ya Maksai

Maksai wanatakiwa kutunzwa na kulishwa vizuri ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

KUWALISHA

Maksai hufanya kazi nzito hivyo lazima wapate chakula cha kutosha. Walishwe majani makavu kiasi cha asilimia 10 ya uzito wake. Pia wapewe vyakula vya ziada vya mchanganyiko wa pumba, mashudu na madini. Wapewe maji safi ya kutosha kabla ya kwenda na baada ya kurudi kazini.

Hakikisha kuwa chakula cha maksai kinakuwa na viinilishe vyote muhimu ambavyo iu wanga, protini, vitamini na madini.

Chakula bora ambacho huweza kupatikana katika maeneo mengi ni:-

- Nyasi kavu au mbichi
- Mimea jamii ya mikunde
- Nyasi zilizokaushwa kitaalam (Hay)
- Pumba za nafaka kama mtama na mahindi,
- Masaliayakaranga
- Masalia ya mazao kama vile mabua ya mahindi mtama na uwele
- Chumvi au magadi
- Maji safi.

KINGA NA TIBA YA MAGONJWA

Kinga muhimu dhidi ya magonjwa ya maksai ni lishe bora na usafi wa mazingira.

Maksai lazima wapate kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali kama vile sotoka, kimeta na chambavu. Maksai waogeshwe ili kuwakinga na magonjwa yaenezwayo na kupe.

Endapo maksai ataonyesha dalili za kuugua, mkulima amuone daktari wa mifiigo aliye karibu kwa ushauri na tiba.

RATIBA YA KAZI KWA MAKSAI

Maksai wapangiwe ratiba maalum ya kufanya kazi. Ratiba ifuatayo inashauriwa kutumika.

Saa 12.00 - 4.00 Asubuhi

Maksai wafanyp kazi

Saa 4.00 asubuhi - 10.00 Mchana

Maksai wapumzike, wapewe maji ya kunywa na wapelekwe malishoni.

Saa 10.00 - 12.00 Jioni

Maksai wafanye kazi

Saa 12.00 Jioni

Maksai wapumztshwe, wapewe maji ya kunywa na chakula cha ziada.

Muda wa kuanza kazi unaweza kubadilika kulingana na mawio na machweo ya jua. Saa za kufanya kazi zitategemea hali ya hewa na udongo ambapo maksai wanafanya kazi.

Kumbuka:

- Maksai yvapate muda wa kula, kunywa na kupumzika. Wapewe chakulacha ziada.

- Wakufunzi wasiwatishe au kuwaumiza wakati wa kuwafundisha.

- Maksai wasifanyishwe vitendo vya kikatili kama kuwapiga mijeledi bila sababu, kuwauma au kukunja mkia na kuunguza kwa vijinga vya moto.

- Maksai waongozwe kwa amri fupi na waitwe kwa majina yao.

- Maksai wasibadilishwe nafasi zao.

- Maksai waongezewe kazi kulinga na uwezo.

- Maksai wafanye kazi asubuhi na jioni tu kutegemea kazi iliyopo na mazingira.

- Maksai aliyepatiwa kinga au tiba apumzishwe.