Cover Image
close this bookHam volume 8 - Jarida la mabadiliko na uimarishaji wa sekta ya Afya Tanzania (Wizara ya Afya, 1998, 38 p.)
View the document(introduction...)
View the documentViongozi wapya Wizara ya Afya
View the documentTahariri
View the documentChiduo asisitiza umuhimu wa mabadiuko ya sekta ya afya
View the documentMkutano wa waganga wakuu wa mikoa 1998
View the documentMfumo wa afya wa wilaya
View the documentChangamoto mpya kwa afya ya jamii
View the documentMfumo wa taarifa kwa ajili ya uendeshaji
View the documentMagonjwa Mapya ya kuambukiza na yanayojirudiarudia
View the documentUgonjwa wa Kisukari
View the documentMabadiliko ya idadi ya watu Tanzania
View the documentSera ya idadi ya Watu
View the documentIdadi ya Watu na Mazingira
View the documentTaarifa ya ongezeko la Wazee Duniani
View the documentMatatizo ya wazee katika jamii
View the documentUnapata uzoefu gani kutokana na maelezo ya kazi za mganga wa wilaya huyu?
View the documentJitihada za Kimataifa za kupambana na ugonjwa wa Malaria
View the documentShirika la afya duniani na mapambano dhidi ya Ukimwi
View the documentUsalama wa damu ni muhimu kudhibiti ukimwi
View the documentAthari ya Ukimwi Wilayani Makete
View the documentChangamoto za kimaadili na haki za binaadamu zinazowakabili wafanyakazi
View the documentWanawake na watoto ni sehemu muhimu katika jamii
View the documentHuduma ya Wakunga wa jadi Tanzania
View the documentAthari za Tumbaku, pombe na madawa kwa mama mjamzito
View the documentBushi
View the documentMabadiliko ya muundo wa uendeshaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
View the documentKilio cha wakimbizi na maisha ya kifamilia
View the documentWafadhili na Maskini
View the documentMatangazo
View the documentChemsha maji yako
View the documentMaadili ya PCB (Cost of Conduct)
View the documentKisa cha mtaalam wa afya kwa jamii
View the documentKinyume

Idadi ya Watu na Mazingira


Mahusiano Baina ya Idadi ya Watu na Mazingira

Mazingira ni jumla ya mambo mengi ambayo yanahusiana na kuathiriwa moja kwa moja ama vinginevyo na watu. Kwa mfano, upanuzi wa ardhi inayotumiwa kwa uzalishaji wa chakula, pamoja na ufugaji unaweza kuathiri misitu yetu na wanyama pori. Vile vile tunaharibu misitu kwa kukata miti kwa ajili ya kuni. Zaidi ya kutupatia mnishati, misitu inaweza kuathiri upatikanaji wa maji, na ikiharibiwa inaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo. Mmomonyoko wa udongo kwa upande mwingine unaathiri uwezo wa kuzalisha chakula. Idadi ya watu inavyoongezeka kwa haraka inaweza kusababisha na kuharakisha uwiano usioridhisha katika mazingira, na kuleta mafatizo makubwa kwa kila mtu.

Matumizi ya Ardhi na Uharibifu wa Mazingira

Kwa vile Tanzania ni kubwa na kuna tofauti za kimaumbile kutoka sehemu moja hadi nyingine, hapajawa ufumbuzi wa kudumu juu ya uharibifu wa mazingira na kupungua kwa rasilimali ya ardhi. Wizara ya Ardhi, Mali Asili na Utalii, katika mpango wa uendelezaji Misitu kwa kipindi cha mwaka 1990-2008, imeainishwa kanda maalum zinazohitaji kushughulikiwa.

· Katika sehemu ya Usambara Magharibi, miteremko ya milima Kilimanjaro, Meru, pamoja na Wilaya za Kagera, Rungwe, Ukerewe Tarime na Mbulu, kuna msongamano mkubwa wa watu na matumizi makubwa ya ardhi kwa ajili ya kilimo na miti kwa ajili ya kuni, jambo ambalo linasababisha kutoweka kwa misitu. Sehemu hizi vile vile zinakabiliwa na uwezekano mkubwa wa mmomonyoko wa udongo kutokana nna maumbileyake na mvua nyingi.

· Maeneo ya Mwanza, Mara na baadhi ya sehemu za Shinyanga yanaathiriwa n a ongezeko la haraka la idadi ya watu na kilimo cha pamba pamoja na ufugaji usioambata-na na uwezo wa malisho.

· Mbuga za Masai, pamoja na sehemu za mikoa ya Dodoma na Singida zinaathiriwa sana naufugaji wa mifugo mingi kuliko uwezo wa malisho unaotokana na wafugaji wanaohama kutoka sehemu moja hadi nyingine.

· Mkoa a Tabora pamoja na Wilaya za Chunya na Iringa Kaskazinizinaathirika sana kutokana na kilimo na uzalishaji wa Tumbaku.

· Mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa Kusini na Ruvuma Magharibi ndizo sehemu zinazozalisha chakula kingi Tanzania, zikizalisha mahindi kwa ajili ya biashara.

· Maeneo ya Kigoma - Mpanda na Rukwa Kaskazini yanakab-iliwa na msongamano mkubwa wa watu kutokana na idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda, ambao vile vile wanahitaji ardhi kwa ajili ya kilimo.

· Maeneo ya Dodoma yaliyoko chini ya mpango wa HADO, na sehemu za Shinyanga zilizoko chini ya mpango wa HASHI zimeathirika sana.

· Katika ukanda wa Pwani na Visiwa vya Mafia, utengenezaji wa chumvi pamoja na ukaushaji wa samaki kwa kutumia kuni, vimesababisha uharibifu wa misitu, na hasa misitu ya mikoko.

· Katika sehemu za Morogoro Mashariki, Mkoa wa Pwani isipokuwa Rufiji Magharibi ya Tanga na kusini Mashariki ya Mkoa wa Dodoma misitu imefyekwa sana kutokana na mahitaji ya miti kwa ajili ya mkaa na kuni.

· Sehemu za Lindi, Mtwara, Ruvuma Mashariki, Morogoro na Kusini na Kusini mwa Mkoa wa Pwani ambako msongama-no wa watu ni ndogo, misitu, bado inastawi vizuri na kuna miti mingi. Lakini, hata sehemu hii vile vile bado iko katika tishio la kuharibiwa iwapo hatua za haraka za kuhifadhi misitu hii hazitachukuliwa.