Cover Image
close this bookHam volume 8 - Jarida la mabadiliko na uimarishaji wa sekta ya Afya Tanzania (Wizara ya Afya, 1998, 38 p.)
View the document(introduction...)
View the documentViongozi wapya Wizara ya Afya
View the documentTahariri
View the documentChiduo asisitiza umuhimu wa mabadiuko ya sekta ya afya
View the documentMkutano wa waganga wakuu wa mikoa 1998
View the documentMfumo wa afya wa wilaya
View the documentChangamoto mpya kwa afya ya jamii
View the documentMfumo wa taarifa kwa ajili ya uendeshaji
View the documentMagonjwa Mapya ya kuambukiza na yanayojirudiarudia
View the documentUgonjwa wa Kisukari
View the documentMabadiliko ya idadi ya watu Tanzania
View the documentSera ya idadi ya Watu
View the documentIdadi ya Watu na Mazingira
View the documentTaarifa ya ongezeko la Wazee Duniani
View the documentMatatizo ya wazee katika jamii
View the documentUnapata uzoefu gani kutokana na maelezo ya kazi za mganga wa wilaya huyu?
View the documentJitihada za Kimataifa za kupambana na ugonjwa wa Malaria
View the documentShirika la afya duniani na mapambano dhidi ya Ukimwi
View the documentUsalama wa damu ni muhimu kudhibiti ukimwi
View the documentAthari ya Ukimwi Wilayani Makete
View the documentChangamoto za kimaadili na haki za binaadamu zinazowakabili wafanyakazi
View the documentWanawake na watoto ni sehemu muhimu katika jamii
View the documentHuduma ya Wakunga wa jadi Tanzania
View the documentAthari za Tumbaku, pombe na madawa kwa mama mjamzito
View the documentBushi
View the documentMabadiliko ya muundo wa uendeshaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
View the documentKilio cha wakimbizi na maisha ya kifamilia
View the documentWafadhili na Maskini
View the documentMatangazo
View the documentChemsha maji yako
View the documentMaadili ya PCB (Cost of Conduct)
View the documentKisa cha mtaalam wa afya kwa jamii
View the documentKinyume

Matatizo ya wazee katika jamii

Maisha ya binaadamu ni hatua inayoanza na kuzaliwa kwa mtolo anaendelea kukua hadi kufikia uzee, hatua ambayo siyo tu inakuwa tegemezi kama ile ya mawazo, bali pia ni ngumu kukabiliana nayo hasa katika mataifa maskini duniani.

Wazee kama walivyo watoto wadogo, wanatakiwa kupewa uangalizi mkubwa hasa upandewa lishe na huduma za afya. Mzee akipata lishe nzuri na huduma nzuri za afya tangu utotoni, hatapata matatizo makubwa katika hatua za mwisho wa maisha yake.

Bila jitihada hizi kufanyika, Taifa linaweza kujikuta linakuwa na wazee wengi wasiojiweza ambao afya za mwili zinahitaji gharama kubwa kuzitunza.

Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, katika nchi zinazoendekea, theluthi mbili ya watu katika nchi hizo ni watu wazima na inakisiwa kuwa idadi hiyo itaongezeka na kufikia robo tatu katika miaka michache ijayo.

Taarifa zinasema katika Bara la Afrika, Nigeria ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wazee wanaokadiriwa kufikia zaidi ya watu 16 milioni wenye umri zaidi ya miaka 60 ifikapo mwaka 2025.

Kutokana na maumbile yao kiafya na kiakili, hali zao za kiuchumi na mazingira yenyewe, wazee wanahitaji malezi makini zaidi ya jamii na hasa huduma bora za afya.

Kwa vile miili ya wazee hudhoofika, huweza kuathinwa kirahisi na magonjwa na hasa kwa wazee wanaoishi vijijini ambakohuduma za afya ni duni.

Pamoja na hali yao hiyo, wazee wa vijijini kuendelea kufanya kazi ngumu za kilimo, kutafuta kitoweo, maji, na kutafuta kuni katika umbali mrefu na hivyo kufanya afya zao ziendelee kuzorota zaidi.

Katika hali ya ubinadamu na mazoea, utakuta wazee wanashiriki kuchangia kipato cha familia kwa ukarabati vibanda au nyumba zao na kulima. Katika hali halisi, ni sehemu chache sana vijijini zinazotenga chakula kwa ajili ya wazee.

Inasikitisha kukuta katika sehemu zingine za vijiji vyetu, wazee wameachwa na wajukuu zao na wazazi wao kukimbilia kile wanachoita maisha. Katika hali ya namna hiyowazee huachiwa mzigo wa kuwatunza watoto bila msaada wa angalau wa kifedha kutoka kwa wazazi wa watoto waliokimbilia mjini.

Kwa vile huduma za afya katika vijiji vingi zinapatikana katika umbali wa kati ya kilo mita 5-10 wazee ambao hawamudu kutembea umbali huo hawafaidiki na huduma hizo.

Baadhi ya magonjwa ambayo huwaumbua sana wazee ni pamoja na yale ya macho kama vile ‘Cataract’, ‘Glaucoma’ na ‘Trachoma’, na ‘vichomi’ na TB, na magonjwa ya moyo.

Mengine ni kisukari, kansa, shinikizo la damu, magonjwa ya mifupa na misuli kama vile ‘Arthritis’ na ‘Rheumatism’ na magonjwa ya akili.

Kuna haja kwa Taifa kuondoa mikakati ya mipango ya dhati inayolenga kuwahudumia kikamilifu wazee kwa kuandaa malezi bora kwa ajili yao na hasa kwa kuhakikisha kwamba wanapata lishe nzuri na huduma bora za afya.

Hata hivyo, mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi, hali kadhalika, wanaweza kupanga mipango na taratibu nzuri za kuwahudumia wazee.

Miaka ya nyuma wazee walikuwa wanatunzwa na ndugu zao au na jamii kwa ujumla. Hali ilivyo sasa ni ya shida sana kwa wazee, utakuta wanawatoroka, wanakimbilia mijini na kuwaacha wazee vijijini, je? hili ni jambo la maadili kweli?

Uzee sasa unaogopwa kwa wasiwasi wa kutotunzwa na hivyo kubaki katika hali ngumu ya maisha na kuachwa unakufa peke yako. Katika karne mpya inayokuja, ni vyema kuweka mikakati ya kuwasaidia wazee kama maadili yetu yanavyotuagiza.


Kukua na hatimaye kuzeeka