
| Ham volume 8 - Jarida la mabadiliko na uimarishaji wa sekta ya Afya Tanzania (Wizara ya Afya, 1998, 38 p.) |
Kutoka Kitengo cha Huduma ya Afya ya Uzazi na Uhai wa Mtoto
Huduma za Afya ya Uzazi hutolewa katika vituo vya huduma za afya na jamii. Lengo Kuu la huduma hizi ni kuimarisha na kuboresha afya za wanawake wenyewe wenye umri wa kuzaa watoto na vijana, pia kupunguza madhara yatokanayo na matatizo ya uzazi na idadi ya vifo kwa makundi haya muhimu.
Licha ya kusambazwa kote nchini kwa huduma hizi lakini bado vifo vitokanavyo na uzazi vinaendelea kuwepo kwa kiwango kikubwa ijapo vinaweza kuzuilika. Takwimu zinaonyesha kuwepo kwa wastani wa wanawake 529 kwa kila laki moja ya watoto wanaozaliwa hai hufa kila mwaka.
Katika kutambua umuhimu wa huduma za wakunga wa jadi katika jamii, Serikali ilianzisha mafunzo rasmi kwa wakunga wa jadi mnamo mwaka 1986. Lengo la mafunzo likiwa nikuboresha huduma wanazozitoa.
Mkunga wa jadi kwa kawaida ni mwanamke wa makamo mwenye uwezo wa kupima mimba, kutoa ushauri na kuzalisha, ambaye amekubaliwa na kutambulika na jamii anamoishi. Uzoefu wake wa kuzalisha unatokana na kurithi au kwa kufanya kazi na wanawake wanaozalisha nyumbani.
Mkunga wa jadi kama atashirikishwa na kuhusishwa kikamilifu katika utoaji wa huduma za afya ya uzazi, anaweza kuchangia kwa kiwango kikubwa katika kutekeleza lengo la uzazi salama.
Mkungawa jadi aliyepata mafunzo anatarajiwa kufanya yafuatayo:-
Kutuo huduma kwa mwanamke mjamzito
Kuwatambua wanawake wenye matatizo na kuwapa rufaa
Kumusaidia mama wakati wa kujifungua
Matunzo baada ya kuzaa
Kuzuia uambukizo wa magonjwa ya zinaa na UKIMWI kwa mtoto, mama au Mkunga wa jadi wakati wa kujifungua.
Kutoa elimu na ushauri kuhusu afya ya uzazi kwa vijana
Kusaidiakuletamaendeleoya jamii
Utoaji, utumiaji na utunzaji wa taarifa.
Wakunga wa jadi wanahitaji vifaa muhimu vya kufanyia kazi. Wilaya au Taasisi zinazoandaa mafunzo ya wakunga wa jadi zinapaswa kuandaa mapema vifaa hivyo vya kuwasaidia wakunga wa jadi kutekeleza vizuri yale waliyofundishwa. Ni vizuri zana hizo zitumike zile ambazo zinapatikana kwa urahisi katika maeneo yao. Vifaa maalum vinavyohitajika ni pamoja na sabuni, nyembe, nyuzi, vyombovya kuwekea maji na vifaa, mikeka, mipira ya kuvaa mikononi, mpira wa kulalia wakati wa kujifungua taa ya kandili, beseni dogo na kipimio cha kupima urefu (pima futi).