Cover Image
close this bookKitabu cha Mwongozo kwa Wavuvi Wadogowadogo - Namba 5: Utunzaji na Ukarabati wa Vyombo vya Uvuvi (Mbegani Fisheries Development Centre - COSTECH, 60 p.)
View the document(introduction...)
View the documentUTANGULIZI/SHUKRANI
Open this folder and view contents1. SEHEMU YA KWANZA - NAMNA YA KUPANDISHA CHOMBO
Open this folder and view contents2. SEHEMU YA PILI - NAMNA YA KUCHUNGUZA CHOMBO
Open this folder and view contents3. SEHEMU YA TATU - UTUNZAJI NA MATUMIZI YA VIFAA ZANA NA MALIGHAFI (MAUNZI)
Open this folder and view contents4. SEHEMU YA NNE - UUNDAJI WA CHOMBO
Open this folder and view contents5. SEHEMU YA TANO - UPAKAJI RANGI
Open this folder and view contents6. SEHEMU YA SITA - UPAKAJI SIFA NA SHAHAMU
Open this folder and view contents7. SEHEMU YA SABA - NAMNA YA KUSHUA CHOMBO
Open this folder and view contents8. SEHEMU YA NANE - USHONAJI WA TANGA
View the document9. FAHARASA

UTANGULIZI/SHUKRANI

Mashua kwa jina la kitaalamu hujulikana kama chombo. Hivyo vinajumuisha mtumbwi, ngalawa, mashua, jahazi, dau na kadhalika.

Vyombo hivi hutumika katika nyanja mbali mbali k.m. kuvulia, usafirishaji wa abiria au mizigo na hata kufanyia michezo ya majini.

Uundaji wa chombo huwa kwa kutumia mbao, chuma, utembo kioo (fibreglass) au maunzi ya aloi saruji (ferro cement).

Ili chombo kiweze kudumu kinahitaji mambo makuu mawili nayo ni:

1. Utunzaji mzuri
2. Ukarabati

Kitabu hiki kimelenga katika mada hizo mbili na ni matazamio yetu kwamba kitawahamasisha na kuwasaidia wavuvi katika kufanya marekebisho madogo madogo yanapotokea kwa kutumia vyombo au vifaa vichache tu na inaposhindikana ndipo atafutwe mtaalamu wa fani hiyo.

Maelezo mengi yametilia mkazo kwenye vyombo vya mbao na yatawagusa takribani wavuvi wote wa maji chumvi na maji baridi.

Pia napenda kutoa shukrani kwa wale wote walioshiriki katika maandalizi ya mtaala huu hasa Nd. J. Shilla katika kutayarisha baadhi ya mada zilizomo ndani pia walimu wa Chuo cha Uvuvi Liuli, vituo vya kozi fupi za uvuvi Pangani na Musoma katika kutoa maoni yao baada ya kupitia sawidi ya mtaala wa awali. Pia Bi Esther Mweyo kwa uchapishaji wa wa kitabu hiki.

Kwa vile itaniwia vigumu kumtaja kila mtu mmoja mmoja, ningeomba shukrani hizi ziwaendee wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wamechangia katika maandalizi ya kufanikisha kazi hii. Ni matumaini yangu kwamba mtaala huu ni kama kianzio tu na marekebisho yatazidi kufanywa ili kupata kitu kamili.

Hivyo basi tutafurahi kupokea maoni na ushauri zaidi kwa wale watakaoutumia mtaala huu kwa kufundishia.

G. L. Shirima
Idara ya Ujenzi wa Mashua
Mbegani Chuo cha Maendeleo ya Uvuvi
Bagamoyo.
Desemba, 1989