Cover Image
close this bookKitabu cha Mwongozo kwa Wavuvi Wadogowadogo - Namba 5: Utunzaji na Ukarabati wa Vyombo vya Uvuvi (Mbegani Fisheries Development Centre - COSTECH, 60 p.)
close this folder4. SEHEMU YA NNE - UUNDAJI WA CHOMBO
View the document(introduction...)
View the document4.1. Kukwangua
View the document4.2. Ubadilishaji mbao mbovu Mbao za mbavuni/mataruma
View the document4.3. Mbao za Mbavuni
View the document4.4. Kigezo
View the document4.5. Kukarabati Ubao
View the document4.6. Kukarabati Mataruma
View the document4.7. Mataruma Tabakishwa
View the document4.8. Mataruma Kingoe
View the document4.9. Mataruma Pasuliwa
View the document4.10. Njia za Kukarabati
View the document4.11. Kiungo Liwato
View the document4.12. Kiungo Sulu
View the document4.13. Nusu - Kiungo Sulu

4.1. Kukwangua

Hatua ya kwanza baada ya chombo kupandishwa na kuwekwa katika sehemu yake ya kazi ndani ya banda ni ukwanguaji wa ubao au mwili wa chombo kwa nje.

Ukwanguaji huu hufanyika kwa kutumia aidha kigwanguzi. Shabaha au lengo kuu la ukwanguaji ni kuondoa takataka na machaza ambayo yamegandamana katika mwili wa chombo. Faida kubwa ya ukwanguaji ni kumwezesha fundi anayekarabati kuweza kugundua ubovu uliofichwa kwa rangi au takataka za machaza. Baada ya hatua hii ya ukwanguaji, hatua inayofuatia ni ubadilishaji wa mbao mbovu.