
| Utenzi wa Nyakiiru Kibi (ECOL Publications, 1997, 109 p.) |
|
Nyakiiru Kibi ni miongoni mwa mashujaa mashuhuri wa Afrika Mashariki walioasisi enzi mpya zilizobadili mkondo wa historia ya jamii zao. Alikuwa ni wa ukoo wa Babito. Alitokea Bunyoro, Uganda na kuhamia katika ufalme wa Kiziba, Bukoba, katika karne ya 15. Kwa ujanja, akili na silaha, kijana huyu, alifanikiwa kujifanya mtawala wa Kiziba, na hivyo kuanzisha ufalme wa Kibito uliodumu kwa karne nyingi. Utenzi huu unasimulia kisa cha mfalme huyu shujaa, ambaye hekima, ukarimu na ujasiri wake ungali unakumbukwa hadi leo.
Mtunzi wa utenzi huu, Mugyabuso M. M. Mulokozi ni mtafiti Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alizaliwa tarehe 7 Juni, 1950. Pia ameandika vitabu vifuatavyo:
Mashairi ya Kisasa (pamoja na K. K. Kahigi)
Malenga wa Bara (pamoja na K. K. Kahigi)
Mukwava wa Uhehe (Tamthiliya)
Kunga za Ushairi wa Diwani Yetu (pamoja na K. K. Kahigi)
Ngome ya Mianzi (Riwaya)
Ngoma ya Mianzi (Riwaya)
Moto wa Mianzi (Riwaya)
MRADI WA VITABU VYA WATOTO
ISBN 9987 397 04 1
ECOL Publications
People with Technology
Printed by Mzumbe Book
Project