![]() | Fasihi, Uandishi na Uchapishaji (Dar Es Salaam University Press, 1993, 260 p.) |
![]() | ![]() | SEHEMU YA KWANZA: UWAVITA |
I.C. Mbenna
1. Vyama vya waandishi sio wazo geni katika nchi yetu. Hata wakati wa ukoloni vijana shuleni waliunda au walishawishiwa na waliniu wao kuunda vikundi vya waandishi wa gazeti la shule, michezo ya kuigiza, vichekesho, mashairi na kadhalika. Tofauti iliyopo ni kwamba hawakuhimizwa kuendelea na vikundi hivyo baada ya kumaliza masomo yao. Zaidi ya hayo, mawazo yaliyopendelewa zaidi ni yale ya kutukuza ukoloni, nadharia na starehe tu.
2. Watu wachache waliodiriki kuendelea na uandishi kwa ajili ya magazeti na vitabu, kwa mfano, Shaaban Robert, A. Abedi Kaluta na Mathias Mnyampala hawakupata tuzo linalostahili kwa kazi yao, na walikuwa mara nyingi katika hatari ya kushtakiwa au kushutumiwa na serikali ya kikoloni.
3. Miaka michache tu baada ya kupata uhuru na kuwa na serikali yetu, Watanganyika wachache waliokuwa wakiishi Dar es Salaam walijiunga na kuanzisha chama cha waandishi kikiitwa "Tanzania Writers Association." Kwa kuwa waliokuwa na uwezo wa kuandika vitabu walikuwa wachache sana, chama hiki hakikujulikana na hakikuhimili misukosuko.
4. Hata hivyo baadaye walijitokeza wananchi wengine wenye upenzi na mashairi wakaunda chama chao "UKUTA" (Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania). Bado chama hiki kinajikokota pamoja na matatizo yake ya fedha.
5. Vuguvugu lilikuwa kubwa aidi mnamo mwaka 1974 wakati vijana wachache, wafanyakazi Dar es Salaam, walipojiunga na kuanzisha chama "WAANDISHI WA VITABU TANZANIA (WAVITA)." Kiliongozwa na Ndugu I.C. Mbenna (Mwenyeldti), Ndugu Rashid Sdf (Makamu Mwenyekiti), Jumaa Mkabarah (Katibu), J.P. Mbonde (Mwekahazina).
6. Maombi ya kuandikisha chama yalipelekwa Machi 1974 kwa Msajili wa Vyama, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wizara zinazohusika zilikaa na maombi hayo hadi 24 Februari, 1976 kilipopewa hati Na. So. 5908.
7. Mnamo mwanzoni mwa 1977 kikajitokeza kikundi kingine katika mji wa Dodoma. Kikundi hicho kilikuwa kikiongozwa na Ndugu Shemshanga. Na shabaha yake ilikuwa ileile ya kuwaunganisha waandishi wa vitabu na kuwahimiza waandike. Kikundi hicho kilijiita "UMOJA WA WAANDISHI VITABU TANZANIA (UWAVITA)"
8. Kwa bahati njema wakagundua kuwa kipo chama kingine Dar es Salaam; na kwamba si vyema kuzusha vikundi mbalimbali vyenye shabaha na lengo moja.
9. Jitihada zikafanywa kukutanisha vikundi viwili hivyo ili kuunda chombo kimoja kitaifa. Makubaliano yalipatikana na maombi ya kubadili jina na katiba yakatumwa kwa Msajili wa Vyama tarehe 23.3.1977.
10. Kabla Msajili hajakubali mabadiliko hayo, ikafahamika kuwa kuna kikundi kingine kilichokuwa kikitaka kuandildshwa tangu 1975 hadi 1978 na kilikuwa bado kupata hati. Kikundi hicho kilijiita "UMOJA WA WAANDISHI NA WAFASIRI VITABU TANZANIA (UWAVITA)." Kikundi kiliongozwa na Ndugu F.F. Kawegere na Abass Abdallah Ishabailu huko Mwadui, Shinyanga. Masjala ya vyama ikatataoishwa na kufanana kwa majina na katiba, na ikawa vigumu kuvitofautisha vikundi hivyo.
11. Kwa bahati nzuri, vikundi hivi viwili vikakubaliana, chini ya ushauri wa Msajili wa Vyama, kuungana tarehe 10.10.1978. Katiba mpya ikaandaliwa na jina likawa UMOJA WA WAANDISHI WA VITABU TANZANIA (UWAVITA) na kuandikishwa upya tarehe 17.8.1979.
12. Viongozi wa awali walikuwa:
Mwenyekiti: |
Ndugu Leonard John Kawala |
Makamu Mwenyekiti: |
Ndugu Euphrase Kezilahabi |
Katibu Mkuu: |
Ndugu Irenei Cassian Mbenna |
Mweka Hazina: |
Ndugu Dadi Mwaware |
Mlezl: |
Ndugu Ibrahim Kaduma |
Wadhamini: |
Ndugu Ezekiel Kaungamno |
|
Ndugu Nazareno Ngulukulu |
13. Baada va kufanya marekebisho machache katika Katiba. uchaguzi wa viongozi ulifanyika tarehe 16.3.1985 na 11.4.1987. Nafasi zilizojazwa ni kama ifuatavyo:
Mwenyekiti: |
Ndugu Euphrase Kezilahabi |
Katibu Mkuu: |
Ndugu Irenei Cassian Mbenna |
Mwekahazina: |
Ndugu Richard Mabala |
Mhariri Mkuu: |
Ndugu M.M. Mulokozi |
Katibu Mwenezi: |
Ndugu H.G. Mwakyembe |
14. UWAVITA ni chama pekee kitaifa na matawi yanaweza kuanzishwa popote Tanzania. Matawi ya kwanza yalikuwa Dar es Salaam, Mwadui na Dodoma. Sasa yamebakia Dar es Salaam na Kigoma. Mengine yamekufa kutokana na kuhama kwa wanachama.
15. Kwa upande wa ushirikiano na vyombo vingine, UWAVITA kimewakilishwa na Katibu Mkuu, Ndugu Mbenna, katika mkutano wa kimataifa wa "Afro-Asian Writers Association " huko Urusi, Aprili 1979; na katika semina ya kimataifa ya Kiswahili iliyoendeshwa na TUKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1978 na 1980. Zaidi ya hayo kimetembelewa na mwandishi wa Kirusi, Komredi Nickolai A. Anastasyev na waandishi wengine wa Urusi, Uchina na Misri.
Semina ya waandishi ya tarehe 26.10.87 hadi 29.10.87 imefanyika kutokana na misaada na ushirikiano wa vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa. Watu, vyombo na mashirika hayo ni pamoja na:
(i) Baraza la Kiswahili la Taifa
(ii) Balozi Yusushi Kurokochi wa Japan
(iii) Profesa Hino wa Japan
(iv) Ubalozi wa Ujerumani Magharibi (FRG)
(v) Waandishi wa Japan
(vi) Ubalozi wa China
(vii) Ubalozi wa Norway (NORAD)
(viii) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Utamaduni, Vijana na Michezo.
16. Mipango iliyokusudiwa katika utekelezaji wa malengo na madhumuni ya umoja ni:
(a) Kuanzisha na kuendesha jarida liitwalo FARAJA.
(b) Kutangaza chama na kuwaandikisha wanachama zaidr.
(c) Kuanzisha matawi.
(d) Kuendelea kupokea, kusoma na kuhariri miswada ya wanachama.
(e) Kuhimiza michango.
(f) Kufanya mikutano mara kwa mara kikatiba.
(g) Kubuni na kuendesha miradi ya uandishi, uchapaji na uchapishaji. (h) Kuendesha semina au warsha.
(i) Kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kusoma, uandishi wa vitabu na sanaa zinazoambatana nazo kwa njia ya redio na magazeti.
17. Orodha ya wanachama waanzilishi:
1. L. J. Kawala |
- Kigoma |
2. D. Mwaware |
- Dar es Salaam |
3. Jumaa Mkabarah |
- Muheza |
4. Ali Keto |
- Dar es Salaam (TRC) |
5. Simon Malya |
- Dar es Salaam |
6. Sentore |
- Dar es Salaam |
7. S.K. Msuya |
- Tengeru |
8. Tigiti S. Sengo |
- Dar es Salaam (Chuo Kikuu) |
9. S. Kiango |
- Dar es Salaam |
10. E. Mwasada |
- Dar es Salaam (Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima) |
11. J. Mbonde |
- Iringa (CCM) |
12. J. Rutayisingwa |
- Dar es Salaam (UHURU) |
13. N. Kuboja |
- Mwanza |
14. E. Kaungamno |
- Dar es Salaam (TLS) |
15. Cuthbert Omari |
- Dar es Salaam |
16. May Matteru |
- Dar es Salaam |
17. E.N. Busyanya |
- Dar es Salaam |
18. Penina Mlama (Bibi) |
- Dar es Salaam (Chuo Kikuu) |
19. Pius Ngeze |
- Musoma |
20. S. Shemsanga |
- Dodoma |
21. A. Rajabu (Bibi) |
- Dodoma |
22. Padre John Kabeya + |
- Tabora |
23. Dr. Mongi |
- Tabora |
24. Mchungaji Magongo |
- Moshi |
25. Mchungaji E. |
- Morogoro |
26. Hassani |
- Dodoma |
27. Tessua |
- Dodoma |
28. Miti |
- Dodoma |
29. Yusuf Halimoja |
- Dar es Salaam |
30. Ernest Ambali |
- Dar es Salaam (Daily News) |
31. A.H. Sakara |
- Dar es Salaam (AEP) |
32. L. Mtesigwa (+) |
|
33. I.C. Mbenna |
- Dar es Salaam (Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima) |
34. Amos N. Madalla |
- Sokoine University |
35. Euphrase Kezilahabi |
- Dar es Salaam (Chuo Kikuu) |
36. Mary Margareth (Bi) |
- Dar es Salaam |
37. Tobias Ndyeune |
|
38. Kulikoyela K. Kahigi |
- Dar es Salaam (Chuo Kikuu) |
39. Joseph John Chambo |
- Dar es Salaam |
40. Kandaga J. Muhanga |
- Dar es Salaam |
41. Fatuma Friday (Bi) |
- Dar es Salaam (Taasisi ya Elimu Watu Wazima) |
42. S.D. Irira |
- Dar es Salaam (BAKITA) |
43. M. Mulokozi |
- Dar es Salaam (Utamaduni) |
44. Minaeli Mdundo (Bi) |
- Dar es Salaam (JWTZ) |
45. Estonic K.S. Monyo |
- Arusha |
46. Joe Mnyune |
|
47. Alex Michael |
- Mwanza |
48. Makumbuli Kamtande |
- Mbeya |
49. Kabuterana Mbehoma |
- Korogwe |
50. William Nnonjela |
|
51. Joseph J. Kasanga |
- Urambo |
52. Sufiani H. Shekoloa |
- Mwanza |
53. N.E.R. Mwakasungula |
- Iringa |
54. Z.M.N. Jumbe |
- Dar es Salaam |
55. Marseli J. Heleli |
- Arusha |
56. Stanslaus T.P. Bashungwa |
- Mwanza |
57. Hamidu Usantu |
- Sumbawanga |
58. Bernard Mdeka |
|
59. Athumani J.A. Iluya |
- Musoma |
60. Katavo Enea Mshana |
- Dar es Salaam |
61. Romward Mtabi |
- Dar es Salaam |
62. Mac Elican Obadia |
- Dar es Salaam |
63. Victor C.M. Mkumbe |
- Dar es Salaam |
64. Evarist Njimba |
- Dar es Salaam |
65. John M. Wendo |
- Bmga |
66. Joaster T. Kisanko |
- Shinyanga |
67. Privatus Karugendo |
|
68. Johnson Petro Machory |
- Mwanza |
68. Peter H. Kimweri |
- Kilosa |
70. Rashid Seif Rashid |
- Pemba |
71. Gaufried C. Issaya |
- Songea |
72. Robert Mfugale |
- Dar es Salaam (Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima) |
73. Dawson Mukanda |
- Dar es Salaam |
74. Abdi A. Mkindi |
- Usangi |
75. Prophily Castory Itumbili |
- Dar es Salaam |
77. Erasto Z.M.Z. Mbiling'i |
- Arusha |
78. Mathias A.L.L. Ganyara |
- Dar es Salaam |
79. Enesmo N.N. Bulali |
- Manyoni |
80. Ansgar William Makangamko | |
81. Dellys K. Mihambo |
- Dar es Salaam |
82. Agripinus Mahanya |
|
83. Jeff A. Okinda |
|
84. G.S. Liwenga |
- Songea |
85. M.D. Sahala |
- Arusha |
86. Anderson Bidya |
- Kasulu |
87. Martin N. Katasya |
- Dar es Salaam |
88. M.A. Mtengula (Bi) |
- Dar es Salaam |
89. R. Simbakalia (Bi) |
- Dar es Salaam |
90. E. Mbogo |
- Dar es Salaam |
91. A.A. Ishabailu |
- Mwadui |
92. F.F. Kawegere |
- Bukoba |